fbpx

Tarehe Ya Kuzinduliwa Gari La Apple La Kujiendesha Lenyewe Yasogezwa Mbele!

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Kama wewe ni mfuatiliaji mzuri sana wa TeknoKona utakuwa unajua kuhushiana na gari la kujiendesha lenyewe kutoka Apple (iCar?).


Kama ulipitia swali la hapa basi jibu lake ni 2021. Na sababu za kusogezwa mbele kwa muda zipo nyingi tuu lakini ile kubwa ni kwamba kampuni inaboresha teknolojia ambayo italiwezesha gari hilo kuweza kujiendesha lenyewe

gari la apple
Mainjinia wa gari la kujiendesha lenyewe kutoka Apple (The Sumner brothers) wamesema kuwa wanatengeneza Software ambayo itachukua taarifa nyingi sana ambazo kila gari la Apple litazalisha.

INAYOHUSIANA  Vivinjari (Browser) 5 Bora Katika Vifaa Vya Android!

Ili kuwezesha hili basi kampuni la Apple inabidi liwe na ‘Server’ kubwa sana ili kuhifadhi taarifa. Inasemekana kuwa gari ya kujiendesha yenyewe ina uwezo wa kuchukua taarifa (data) mpaka kufikia GB 10 kwa kila maili itakayo tembea.

Sababu nyingine ya kusogezwa mbele kwa tarehe hiyo ni kwamba kiongozi ambae alikua anaongoza zoezi/mchakato mzima wa magari ya kujiendesha yenyewe kutoka Apple, Steve Zadesky alipata matatizo binafsi na kuondoka na hiyo ilipelekea uongozi mpya kuchaguliwa ili kumrithi.

INAYOHUSIANA  Kosa la kiusalama katika iPhone 6s lagunduliwa

gari la apple
Apple wanakwepa kujibu maswali mbalimbali kuhusiana na teknolojia yao ya magari ya kujiendesha yenyewe. Cha msingi ni kusubiria taarifa rasmi kutoka kwao wakitueleza yale yanayoendelea kujiri.

Kama kawaida yetu tutaendelea kukujuza yale yanayojiri katika utengenezaji wa magari haya. Endele kutembelea TeknoKona ili usipitwe.

MUHIMU: Picha Zote Za Gari Ni Za Kufikirika (Haimaanishi kuwa ndio muundo wa gari)

TeknoKona ndio mtandao wako namba moja kwa habari na maujanja yote ya teknolojia Tanzania. Kumbuka TeknoKona Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comments are closed.