fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

apps Intaneti Spotify

Spotify kupatikana Tanzania, ni habari njema kwa wapenda muziki

Spotify kupatikana Tanzania, ni habari njema kwa wapenda muziki

Baada ya muda mrefu wa kuwepo huduma ya kustream muziki ya Spotify kupatikana Tanzania na katika mataifa mengine 84 mapya.

Spotify kupatikana Tanzania

Spotify kupatikana Tanzania

 

Kwa kuongeza masoko hayo 85 mapya kutaifanya huduma hiyo kupatikana rasmi katika masoko 178 (Masoko ni nchi na mataifa).

Nje ya Tanzania, huduma hiyo itaanza kupatikana kwa mara ya kwanza kwenye nchi nyingine kama vile;

Angola, Antigua and Barbuda, Armenia, Azerbaijan, Bahamas, Bangladesh, Barbados, Belize, Benin, Bhutan, Botswana, Brunei Darussalam, Burkina Faso, Burundi, Cabo Verde, Cambodia, Cameroon, Chad, Comoros, Côte d’Ivoire, Curaçao, Djibouti, Dominica, Equatorial Guinea, Eswatini, Fiji, Gabon, Gambia, Georgia, Ghana, Grenada, Guinea, Guinea-Bissau, Guyana, Haiti, Jamaica, Kenya, Kiribati, Kyrgyzstan, Lao People’s Democratic Republic, Lesotho, Liberia, Macau, Madagascar, Malawi, Maldives, Mali, Marshall Islands, Mauritania, Mauritius, Micronesia, Mongolia, Mozambique, Namibia, Nauru, Nepal, Niger, Nigeria, Pakistan, Palau, Papua New Guinea, Rwanda, Samoa, San Marino, Sao Tome and Principe, Senegal, Seychelles, Sierra Leone, Solomon Islands, Sri Lanka, St. Kitts and Nevis, St. Lucia, St. Vincent and the Grenadines, Suriname, Timor-Leste, Togo, Tonga, Trinidad and Tobago, Tuvalu, Uganda, Uzbekistan, Vanuatu, Zambia na Zimbabwe.

SOMA PIA  Ulinzi waboreshwa kwenye Chrome ya simu

Spotify wamesema pia wanategemea kuongeza shughuli za kuwafikia wanamziki katika maeneo mapya watakayoanza kupatikana ili kuongeza thamani ya kazi kupitia huduma ya Spotify.

spotify

Rasmi lini? Ndani ya siku hizi chache.

Kwa uamuzi huu itegemewe watapata watumiaji wengi katika miezi hii, kwa muda mrefu watumiaji wa Spotify nje ya maeneo rasmi iliwabidi kudanganya katika kufungua akaunti na kwenye kutumia mara nyingi imelazimisha utumiaji wa VPN.

SOMA PIA  Akaunti ya Facebook ya Meya Jerry Silaa Yawa 'hacked'!

Kwa sasa Spotify ina jumla ya watumiaji milioni 345, ikiwa kati ya hao watumiaji milioni 155 ni wa kupitia huduma ya bure (yenye matangazo).

Kwa sasa Boomplay ndiyo app maarufu zaidi Afrika mashariki kwenye huduma ya kustream muziki. Kama vile Boomplay, Spotify inakuja na maktaba kubwa ya muziki pamoja na vipindi vya redio katika mfumo wa Podcast. 

Chanzo: Spotify

SOMA PIA  CHECKY: App Inayokujulisha Umetumia Simu Mara Ngapi Kwa Siku!
Comrade Mokiwa

Comrade Mokiwa

Muanzilishi wa Teknokona na Teknokona Group LTD - WWW.TEKNOKONAGROUP.COM

Muda wangu umegawanyika kati ya kazi kibunifu @teknokonagroup na uandishi wa habari za Teknolojia hapa Teknokona Blog.

| mhariri(at)teknokona.co.tz |

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania