fbpx

Programu tumishi ya Facebook yazidi kutoswa

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Kituo cha utafiti cha Pew kimechapisha ripoti yake kuhusiana na matumizi ya mtandao wa kijamii wa Facebook nchini Marekani.

Kwa mujibu wa matokeo ya timu yao ya utafiti, imeonekana kuwa asilimia 26 ya waliokuwa wakitumia mtandao huo wamefuta ‘programu tumishi ya Facebook katika simu zao katika kipindi cha miezi 12 iliyopita.

Aidha, asilimia ya idadi ya watumiaji waliorekebisha Facebook kwenye simu zao ilikuwa ya juu kiasi cha asilimia 54, wakati asilimia 46 hawajabadili chochote.

Programu tumishi ya Facebook

Matumizi ya mitandao ya kijamii kulingana na kiasi ambacho mtu anitembelea kwa siku.

Dodoso lilifanyika kati ya Mei 29 na Juni 11 na kuwahusisha watumiaji takribani 5000. Kati yao, asilimia 42% hawakutumia kabisa Facebook kwa kipindi cha wiki kadhaa na wengine zaidi ya mwezi.

INAYOHUSIANA  Dell XPS 15: Kompyuta nzuri kwenye uhariri wa picha/video

Kwa ujumla, takribani Mmarekani mmoja kati ya kumi alikuwa amepakua taarifa zote binafsi zilizokusanywa na Facebook. Hata hivyo, kwa kuangalia makundi ya rika, hali hiyo ya matumizi ya Facebook haikuwa na matokeo ya kushangaza.

Kizazi cha vijana kinaonekana kuwa makini zaidi na kuhusiana na matumizi ya mtandao na hivyo, theluthi mbili (2/3) ya vijana waliohojiwa wenye umri wa kati ya miaka 18-29 walibadilisha mipangilio (settings) ya simu zao huku nusu yake wakiifuta kabisa kwenye simu zao.

INAYOHUSIANA  Apple waleta iPhone 6 & 6 Plus , Saa na Mfumo wa Malipo

Kwa upande mwingine, kizazi cha umri wa zaidi ya miaka 65, ni theluthi tu ndiyo waliobadili ‘Settings’ za simu zao takribani zaidi ya asilimia 10 kati yao ndiyo waliofuta programu tumishi ya Facebook.

Programu tumishi ya Facebook

Takwimu za wazee kwa vijana wanaotumia mitandao ya kijamii.

Ripoti inaonyeha kuwa licha ya watumiaji wa mitandao kuendelea kuhama kutoka Facebook, mtandao huo bado una watumiaji wengi zaidi kwa siku ambapo:

katika robo ya pili ya mwaka huu wa fedha (Q2 – 2018) kulinganisha na kipindi kama hiki mwaka uliopita kwa kuwa na wafuasi waliohai (active) kila uchao wanaofikia milioni 185 kwa nchi za Marekani na Canada.

Kwa takwimu hizo, inaonyesha vilevile kwamba kufuta Facebook hakumaanishi kutotumia kabisa mtandao huo wa kijamii – hiyo ikimaanisha kuwa baadhi hufuta ili tu kuokoa matumizi zaidi ya betri kwenye simu zao.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.