Video, sauti na picha za sayari ya masi / mirihi zilizotumwa kupitia misheni mpya ya NASA inayokwenda kwa jina la Perseverance zimeweka rekodi mpya katika teknolojia na mafanikio ya NASA na sekta nzima ya tafiti za kisayari.
Kwa mara ya kwanza, watu wote duniani kupitia simu zetu za mkononi tunaweza kupata picha na video za ubora wa hali ya juu za mazingira ya sayari hiyo.
Si hivyo tuu bali kwa mara ya kwanza pia tumeweza kuona utuaji wa kifaa cha kigari spesheli ulivyofanyika – mara zote shughuli ya kutua kwa kifaa katika sayari hiyo usimamiwa na mfumo wa kompyuta uliokwenye vifaa hivyo – na kutokana na umbali na uchelewaji wa mawasiliano taarifa ya kutua salama au kushindwa huchelewa kufika huku duniani.
Kwa muda mrefu picha za sayari ya masi / mirihi zimekuwa zile zinazotumwa na vifaa vilivyotumwa kwenye sayari hiyo ila zimekuwa si picha ambazo ni za ubora mkubwa wa rangi, kupitia kifaa kipya cha kigari roboti kilichotua kwenye sayari hiyo hivi karibuni mambo yatakuwa tofauti sana. Kigari roboti cha Perseverance kinabeba teknolojia za kisasa kabisa katika upigaji picha, video na sauti – hii ni nje ya teknolojia zingine za utafiti.
Mambo makubwa
- Kwa mara ya kwanza video ya hatua zote za utuaji imeweza kupatikana. Tazama hapa
- Kuna kamera za kisasa zaidi na unaweza pata kutazama panorama ya ubora wa kiwango cha nyuzi 360 hapa.
- Je unataka kusikia upepo wa sayari ya masi / mirihi? Basi sikiliza hapa.
Sauti ya Sayari peke yake
Sauti ya Sayari pamoja na roboti gari Perseverance
Kupitia misheni hii inategemewa watafiti wa NASA na wadau wao wengine wataweza kuifahamu sayari hii kwa mapana zaidi ukilinganisha na miaka ya nyuma. Lengo kuu ni kufahamu kama sayari hiyo ishawahi kuwa na viumbe hai, na ndio basi ni jambo lilitokea.
Katika miaka hii ya karibuni kumekuwa na maendeleo makubwa sana katika teknolojia za sekta ya anga. Mafanikio makubwa yakihusisha SpaceX, NASA na makampuni mengi kadhaa. Endelea kutembelea Teknokona ili usipitwe na habari kama hizi.
Soma pia kuhusu;
Sekta ya Anga – Teknokona/Anga
NASA – Teknokona/NASA
SpaceX – Teknokona/SpaceX
No Comment! Be the first one.