fbpx

Sony waja na kipooza cha kwenye nguo, yaani utatembea na ‘Air Conditioner’ yako

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +

ICT CONFERENCE 2019

Sambaza

Tumezoea kuona vifaa vya kupooza hewa – yaani AC kuwa kwenye majumba, magari na maofisini. Fikiria ya kuweza kutembea nayo popote? Sony waja na kipooza kitakachowekwa ndani ya nguo yako.

Sony waja na kipooza cha kwenye nguo

Sony waja na kipooza cha kwenye nguo

Fikiria unatamani kuvaa suti kwenda kwenye shughuli ya kikazi lakini hali ya hewa hairuhusu, yaani joto ni kali. Hapa ndio teknolojia mpya kutoka Sony inalenga kutatua, nguo yako iwe na kipooza (AC) ndani yake.

INAYOHUSIANA  Zijue Apps Za Picha Na Video Ambazo Ni Mbadala Kwa Instagram Na SnapChat!

Kupitia kitengo chake cha teknolojia za majaribio na zinazokusanyiwa mitaji kupitia mfumo wa uchangiaji kwa wale wanaotaka kununua bidhaa kwa mara ya kwanza (crowdfunding) wamekuja na bidhaa ya kitofauti sana waliyoipa jina la The Reon Pocket.

Sony waja na kipooza cha kwenye nguo

Kitauzwa na shati spesheli. Kifaa hichi kitaanza kupatikana Japani kwanza.

Mfumo huo wa kipooza cha kwenye nguo upo kihivi;

  • Kuna mashati spesheli yatakayokuwa na kama kimfuko kidogo eneo la mgongoni chini kidogo ya shingo.
  • Kupitia kifaa kidogo hicho kitaweza kukaa na chaji ndani ya masaa 24 kwa kuchaji mara moja tuu – kwa muda wa masaa mawili.
  • Kupitia app utakayoweza kuweka kwenye simu yako utaweza kupooza joto lako kwa digrii 4 (C) chini na pia kama kuna baridi sana basi utaweza kuongeza joto kwa kiasi takribani digrii 2 zaidi.
INAYOHUSIANA  Ijue Skateboard Inayoelea Hewani

Lengo la Sony ni kuwezesha baadae app hiyo kuwa na uwezo wa kuweka mpangilio (setting) wa kusimamia kiwango cha joto bila uhitaji wa wewe kufanya chochote, yaani ‘automatically’.

Je una mtazamo gani na teknolojia hii? Tayari maelfu ya watu nchini Japani wameshalipia na watakuwa wateja wa kwanza wa bidhaa hii. Shati na AC yake itauzwa kwa takribani Tsh 200,000/- na zitaanza kupatikana kwa wingi Machi 2020.

Vyanzo: Engadget na tovuti mbalimbali
Facebook Comments

Sambaza

ICT CONFERENCE 2019

Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.