fbpx
apps, Intaneti, Teknolojia, Video, YouTube

YouTube inalipa! Mtoto, Boram anunua jengo la ghorofa 5 la thamani ya dola milioni 8

youtube-inalipa-mtoto-boram-anunua-jengo-la-ghorofa-5-la-thamani-ya-dola-8m

Notice: Trying to access array offset on value of type null in /home/teknoloj/public_html/wp-content/plugins/intelly-related-posts/includes/core.php on line 163
Sambaza

Ushawahi kujiuliza kama YouTube inalipa kwa mambo mengine nje ya muziki na vichekesho? Fahamu mtoto mwenye miaka 6 raia wa Korea Kusini anayefahamika kwa jina la Boram Ki amenunua jengo  lenye thamani ya dola za kimarekani milioni 8 (zaidi ya Tsh bilioni 16) kwa pesa anazotengeneza kwa sababu ya YouTube.

Kwa mujibu wa habari iliyotolewa na shirika la CNN, Boram anaendesha chaneli mbili tofauti katika mtandao wa YouTube akiwa na jumla ya wafuatiliaji zaidi ya milioni 30.

Jengo hilo la ghorofa 5 lipo katika eneo la Gangnam, moja ya maeneo ghari katika jiji la Seoul nchini Korea Kusini.

Kupitia kampuni ya Boram Family iliyoanzishwa na wazazi wake amenunua jengo  hilo kupitia malipo anayoyapata kupitia chaneli zake mbili za YouTube.

INAYOHUSIANA  Hizi hapa simu mbili za Mara X na Z kutoka Rwanda

Katika chaneli hizo mbili za Boram Ki, moja ina wafuatiliaji milioni 13.6 na nyingine ikiwa na wafuatiliaji milioni 17.6 .

Baadhi ya video alizozisambaza kupitia chaneli hizo zimeangaliwa zaidi ya mara milioni 350. Boram huingiza dola milioni 3 kwa mwezi.

Wazazi wengi wanachagua kutumia YouTube kama sehemu burudani kwa watoto wao na hii inafanya akaunti za watoto kuzidi kupata umaarufu na video nyingi zinatazamwa kwa wingi sana. Makampuni ya utengenezaji wa vitu vya kuchezea vya watoto wanachukua nafasi hii kuingia mikataba minono na akaunti hizo.

Katika akaunti zake Boram amekuwa akiweka maudhui ya michezo ya watoto na visa kadhaa vinavyomuhusu vinavyovutia mamilioni ya watazamaji.

INAYOHUSIANA  Tafuta Mtu Yeyote Mwenye Simu kwa Njia Hizi
Ryan Kaji youtube inalipa
YouTube Inalipa: Ryan Kaji ni mtoto wa miaka 7 anayeingiza zaidi ya Tsh Bilioni 44 kwa mwaka kupitia YouTube na mikataba na makampuni ya kutengeneza vitu vya kuchezea vya watoto.

Kwa sasa watoto wamekuwa wakiingiza pesa nyingi kupitia Youtube. Kwa mujibu wa Forbes mwaka jana staa wa YouTube aliyeingiza pesa nyingi zaidi ni Ryan Kaji raia wa Marekani mwenye umri wa miaka saba ambaye aliingiza dola milioni 22.

YouTube inalipa kwelikweli.

Vyanzo: scmp, cnn na tovuti mbalimbali
Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Siyan

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.