fbpx

Samsung Galaxy M30: Simu mpya kutoka Samsung #Uchambuzi

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Samsung Galaxy M30: Samsung wanaleta kitu kipya sokoni kwa ajili ya watu wanaopenda simu yenye ubora mzuri lakini pia bila kuwa na bei ya kuvunja akaunti benki.

Simu hii mpya kutoka Samsung inategemewa kuanza kupatikana nchini India kuanzia tarehe 7 Machi mwaka huu, na baada ya hapo ndio itakuja kwenye nchi zingine. Simu ya Galaxy M30 ni simu ya kwenye kundi la bei za kati na yenye ufanisi mzuri kiutendaji kwa kuwa inakuja na baadhi ya vipuri vyenye sifa nzuri.

INAYOHUSIANA  Betri la simu lenye kizima moto ('fire extinguisher') ndani yake latengenezwa

samsung galaxy m30

Samsung Galaxy M30

Samsung Galaxy M30: Itaanza kupatikana rasmi Machi 2019, kuanzia India na kisha masoko mengine

Simu hii inakuja katika matoleo ya rangi mbili, nyeusi (Gradation Black) na ya blu (Gradation Blue).

Inakuja na kamera tatu nyuma na teknolojia ya kufungua kwa alama za kidole imewekwa eneo la nyuma katikati kwa juu kidogo.

Samsung galaxy m30

Sifa za Samsung Galaxy M30

  • Kuna toleo la GB 4 za RAM ikiwa na diski ujazo wa GB 64, na toleo jingine ni la RAM GB 6 na huku diski ujazo ukiwa wa kiasi cha GB 128.
  • Ukubwa wa display/kioo ni wa inchi 6.4 ikiwa ni ya teknolojia ya FHD+ AMOLED.
  • Kuna uwepo wa kinochi kwa eneo la kamera ya selfi (notch). Kamera ya selfi ni ya Megapixel 16.
  • Inakuja na prosesa (CPU) ya 1.8GHz octa-core.
  • Katika kamera zake tatu za nyuma kuna kamera ya megapixel 13, na kamera mbili ni za megapixel 5 kila moja.
  • Ina betri la kutosha kukaa muda mrefu sana, kwani ni betri la mAh 5000.
  • Uwezo wa memori kadi wa hadi GB 512.
INAYOHUSIANA  Apple kufanyia matengenezo bidhaa zao bure

Bei:

Toleo la RAM ya GB 4 kwa diski uhifadhi wa GB 64 ni $210 (takribani Tsh 500,000), wakati toleo la RAM ya GB 6 kwa diski uhifadhi wa GB 128 ni $252 (takribani Tsh 600,000).

Vipi mtazamo wako juu ya simu hii?

Endelea kutembelea TeknoKona.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.