Kwa kawaida simu janja za Android huonekana kufanana, kwa uchache sana baadhi huonekana mpya. Kwa hakika, kinachobadilishwa mara nyingi ni Kamera kuwa bora zaidi, simu kuwa na kasi zaidi, mara chache na ubora wa battery na uwembamba wa simu, japo ni ngumu kuona. Hakuna kingine cha muhimu.
Japo watengenezaji mara nyingi hutengeneza programu za Adroid kutoka Google, ili kupata upekee wa simu katika mipangilio, lakini utofauti wa matumizi na programu, pengine na maumbo ya nje ya simu hautofautiani sana, licha ya majina ya makampuni kutofautiana kama Samsung, Tecno, Sony LG, BlackBerry au Huawei.
Ni vyema sasa kuangalia simu hizi tatu zinazoendeshwa kwa mifumo ya Android, ambazo zina upekee sana katika maumbo ya nje, tofauti kabisa na simu tunazozijua.
Tunakuletea kwako, 1. BlackBerry Priv ambayo tuliwahi kuizungumzina, simu ya kwanza kabisa ya Blackberry kutumia mfuomo wa Android, yenye sifa ya kuwa na Keyboard ya kawaida, 2. Motorola Droid Turbo 2 ambayo kioo chake kimetengenezwa kutokuvunjika kirahisi kama ikipata ajali, na 3. LG V10 ambayo ina vioo viwili na Kamera mbili za mbele.
Zitazame, tunakuchambulia kwa kina apa chini;
BlackBerry Priv.
Kwa muda sasa, BlackBerry wamekua wakijituma kufanya simu zake kuwa na upekee utakaowapa watumiaji mbadala wa simu za Apple za iPhone na Androids. Japo inaendelea kuandaa mfumo wake peke yake kama wa IOS, lakini kampuni imeamua kutoa simu ya kwanza ya Android.
BlackBerry Priv zina Keyboard za kawaida (sio za kwenye kioo), tofauti na simu nyingi sana za Android. Inaonekana kama simu za kawaida, mpaka utakapotelezesha kioo kwenda juu kama tulivyokua tunafanya kwa simu za Nokia za Kuslide, na kukutana na keyboard yake inayojitegemea. Japo ina keyboard hiyo, lakini simu hzi bado ni nyembamba sana ukilinganisha na baadhi ya simu za Samsung na iPhone.
Vitu vyake vingine vya muhimu ni pamoja na kioo cha nchi 5.4 kilichopindishwa pande zote (Kama S6 Edge), na uwezo mkubwa wa kukaa na chaji kuliko simu nyingi tunazozijua wa zaidi ya masaa 22.5.
Motorola Droid Turbo 2
Motorola wamebadilisha matumizi ya vioo katika kutengeneza kioo cha simu hii, na kuamua kutumia aina fulani ya plastiki maalum kuifanya simu hii kuwa ngumu kuvunjika. Kwa kawaida, simu nyingi zinatumia nyenzo za vioo ambazo huwa nyingi zinapasuka zikiangukia kitu kigumu.
Ni kioo ambacho utaweza kufanya mambo mengi hatari bila kukihofia, kuweka simu mfuko wa nyuma, kuiangusha—- lakini bado simu haivunjiki. Unaweza kuiangusha kutokea umbali mrefu sana, labda vifaa vingine vinaweza kuvunjika lakini si kioo.
Pia, kioo cha simu hii hakikwanguki, kutokana na kutengenezwa kwa material maalum yanayotumia plastiki.
Motorola wamehakikishia watumiaji uhakika wa kutumia adi masaa 48 ya matumizi, huku simu hii ikikupa uwezo wa kutumia kwa masaa 13 kama utaichaji kwa dakika 15.
LG V10
Licha na kuwa na kii kikubwa cha nchi 5.7, lakini bado LGv10 ina kioo kidogo, saizi ya kidole ambayo ni spesheli kwa ajili ya kutoa taarifa za Msingi bila kuingilia kioo kikuu japo taarifa hizo hupotea baada ya sekunde kadhaa.
Kioo hichi cha pili mara zote huwa kimewaka, na kinakupa uwezo wa kufikia sehemu za Msingi kama vile mipangilio ya simu, kamera, majina au App ulizozitumia punde.
V1o ina kamera mbili za mbele, moja kwa ajili ya kupigia Selfie za kawaida na kamera nyingine kwa ajili ya kupigia Selfie za kundi kubwa la watu (Wide Group Selfie) ili kuweza kuwapata wote.. Sifa nyingi za simu hii hazitokelezei kwenye simu nyingine nyingi, hivyo ni kitu bomba kuendelea kuona LG wanagundua vitu vipya.
Tuambie maoni yako?
Chanzo cha Makala haya ni AP
One Comment