Je unaitaji kuchaji simu yako au tableti ata pale ambapo umeme upo mbali nawe, au soketi haipo karibu yako? Basi hii Sony CycleEnergy External Charger itakuwa jibu lako.
Betri hii imetengenezwa kutumia lithiam na itatolewa katika matoleo mawili, la kipimo cha 3,500mAh na la uwezo wa juu wa 7,000mAh. Kupitia toleo ndogo la 3,500mAh lina uwezo wa kuchaji na kujaza simu za kisasa (smartphone) mjazo mmoja na nusu, wakati lile la 7,000mAh lina uwezo wa kuchaji simu ya kisasa zaidi ya mara tatu ndo itaishiwa chaji.
Na kutokana na uwezo huu betri hizi zinachugua muda kuchajiwa, kwa toleo kubwa la 7,000mAh linaitaji kuchajiwa kwa takribani masaa 7 na nusu wakati toleo lingine ni takribani ya nusu ya muda huu.
Kuhusu bei zitauzwa katika bei ya kawaida tuu ambayo ni takribani dola za kimarekani 68 kwa toleo dogo (takribani Tsh 108,800/=), wakati kwa toleo la nguvu zaidi ni dola 89 (Tsh 142,400/=).
Zikiwa zimopokea sifa ya udogo karibia sawa na simu za ‘smartphones’ betri hizi zinategemewa kuingia sokoni mwisho wa mwaka, kuanzia katikati ya mwezi Novemba!
No Comment! Be the first one.