Mawasiliano yangu ya WhatsApp yamekuwa ni rahisi sana kwangu kutokana na uwezo wa kufanya mambo mengi tuu. Na kwa hili la hivi karibuni linanifanya nijisikie furaha kwa kuondoa uwezekano wa kutosoma jumbe hata ikitokea nimesahau nyumbani simu janja yangu.
Kwa haraka haraka ukiwaza ni jumbe ngapi unapokea kwenye WhatsApp ndani ya nusu saa? Na je, huwa inatokea nyingine unasahau kuzisoma? Pengine hukuwa unapenda kutumia WHatsApp kupitia kivinjari au kwa Kiingereza “WhatsApp Web” lakini pengine hili linaweza likakufanya na wewe ukaunganisha simu yako na hivyo ukawa na uwezo wa kupokea na kutuma jumbe bila ya utegemezi wa simu yako ya kiganjani.
Kama hiyo haitoshi unafahamu ya kuwa WhatsApp Web imefanyiwa maboresho na hivi sasa huenda ikawa ni historia kwa watumiaji wake kutokuwa na uwezekano wa kutosoma jumbe walizotumiwa? Ndio, WhatsApp Web imeongezwa kipengele kipya ambacho kinamuwezesha mtumiaji wake kuweza kuchuja na kuona jumbe ambazo hajazisoma.

Tangu kufanyika kwa maboresho hayo nimesahau uwezekano wa kutoona jumbe ambazo sijazisoma kwani kazi kubwa imefanyika nyuma ya pazia kuhakikisha hilo linawezekana kwenye WhatsApp Web. Je, wewe umeshakutana na maboresho hayo? Unayazungumziaje? Tunakaribisha maoni yako ewe msomaji wetu.
Vyanzo: WaBetaInfo, Crast.net
No Comment! Be the first one.