Kwenye ulimwengu wa sasa unazungumzia masuala ya anga la mbali hakika huwezi kuacha kuitaja SpaceX ambayo imekuwa ikifanya mambo mengi kuliko hata ambavyo ilidhaniwa wakati inaanza.Katika kipindi kifupi SpaceX imeweza kuvunja rekodi yake mwenyewe.
Ni miezi saba tu imepita tangu tuanze mwaka 2022 lakini tayari SpaceX imeshavunja rekodi iliyoiweka hadi kufikia mwisho wa mwaka jana. Je, ni rekodi gani hiyo? Hadi kufikia mwisho wa Disemba mwaka 2021, SpaceX walikuwa wamesharusha takribani roketi 31 kwenda anga la mbali. Sasa tupo mwezi Julai na tayari wamefanikiwa kurusha salama mara 32 roketi ya Falcon 9 kwenda anga la mbali.
Nini siri ya SpaceX kuweza kuvunja rekodi yake?
SpaceX inajihudumia yenyewe kwa kupeleka huduma ya intaneti kwenye anga la mbali ili kufanya bidhaa yake yenyewe-Starlink ili kutoa huduma ya intaneti ya kiwango cha juu hivyo kutumia urushaji wa roketi zake kuendeleza kile ilichokipanda huko kwenye anga la mbali.
Lakini hata kama SpaceX wasingekuwa na kazi hiyo bado kampuni hiyo ina makubaliano ya kushikiana na NASA katika kazi zake mbalimbali kama kila baada ya muda fulani hupeleka watu na mizigo kwenye kituo cha kimataifa cha anga la mbali. Vilevile, SpaceX huwa wanakusanya satelaiti ndogondogo na kisha hupelekwa kwenye anga la mbali kwa safari moja.
SpaceX imepanga hadi kufika mwisho wa mwaka 2022 basi wawe wamefanikiwa kurusha kwa mafanikio kwenda anga la mbali takribani mara 52. Na leo (Julai 24) SpaceX intarajiwa kurusha roketi zake nyingine za Starlink kwenda anga la mbali.
SpaceX inaendelea kufanya makubwa tuu ambapo muda bado upo kuonyesha ulimwengu yale ambayo wameyapanga kuyatekeleza mwaka huu.
Vyanzo: The Verge, mitandao mbalimbali
No Comment! Be the first one.