Kama kuna teknolojia ambayo imenufaika sana kutokana na hali ya vita, basi ni teknolojia inayohusisha safari za anga. Roketi ya V2 ni roketi ambayo ilianza kutumiwa na wajerumani katika vita ya pili ya dunia, teknolojia yake imechangia kwa kiasi kikubwa teknolojia za sasa za safari za anga.

Ilikuwaje?
Wakati wa vita vya pili vya dunia serikali ya Ujerumani iliwekeza kwenye utengenezaji wa roketi za kisasa kupitia injia wao Bwana Wernher von Braun ili waweze kushinda vita. Kupitia mabomu yaliyokuwa yanarushwa kupitia roketi za V2 Ujerumani waliweza kusababisha madhara makubwa sana kwa maeneo ya jirani kama vile Uingereza.

Mabomu juu ya roketi ya V2 yaliweza kuchukua muda usiozidi dakika tano kutoka kurushwa hadi kutua umbali wa ata kilometa 190 kutoka liliporushwa. Utofauti wake na rekodi ni kwamba bomu lilsifiri umbali mrefu juu ya anga na kwenda kutua ghafla katika eneo husika na hivyo kuvipa vyombo vya usalama wakati mgumu katika kugundua shambulizi mapema.
Baada ya Vita vya pili vya Dunia, Marekani na taifa la Umoja wa Kisovyeti / Urusi zilipambana vikali katika kuwekeza kwenye teknolojia hii kwani waliamini mwenye roketi zenye nguvu zaidi na za teknolojia ya kisasa atakuwa ndio tishio zaidi kwa mwenzake.
Baada ya Vita vya 2: Marekani
Baada ya vita hivyo Marekani waliwachukua na kuwapa hifadhi timu iliyokuwa inahusika na utengenezaji wa mabomu haya. Timu hiyo ikiongozwa na Bwana Wernher von Braun ndio ikasaidia kwa kiasi kikubwa shirika la anga la NASA katika kufanikisha safari yao ya kwanza ya anga na ata ile ya kutua mwezini. Teknolojia zote za roketi walizokuwa wanazitumia zilikuwa zimebeba misingi ya roketi ya V2.
Baada ya Vita vya 2: Umoja wa Kisovyeti / Urusi
Kwa Urusi wao waliweza kupata mafaili/dokumenti mbalimbali juu ya utengenezaji wa roketi hizi, kupitia kusoma teknolojia hizo wao wakaweza kuwapa kazi watu wao, hii ikiwa ni pamoja na injinia Bwana . Kupitia ubunifu zaidi uliofanywa na Bwana Sergei Korolev, Urusi ndio walishika sifa ya kuwa taifa la kwanza kupeleka chombo cha satelaiti kuzunguka dunia kikiwa anga za juu. Pia Urusi ndio wakawa wa kwanza kupeleka mwanadamu kwenye anga za juu.


Baadae baada ya vita baridi kati ya mataifa haya mawili kuisha wote wakakaa pamoja na kuendelea kushirikiana katika sekta ya tafiti za anga. Na hili ndilo lililoleta chombo cha kimataifa cha anga – kinachozunguka dunia hadi leo. Unaweza kusoma zaidi kuhusu chombo hichi cha anga hapa – Miaka 20 ya Kituo cha Anga cha Kimataifa.
Teknolojia hii imekuja kutoka kwenye jambo baya, mabomu yaliyotumia roketi za V2 yaliua zaidi ya watu 9000 wengi wakiwa raia wa Uingereza, pia utengenezaji wake kwa kutumia watumwa nchini Ujerumani ulisababisha vifo vya zaidi wa watu 12,000 kutokana na milipuko ya bahati mbaya. Nchini Marekani kulikuwa na waliokuwa wanapinga utumiaji wa mainjinia hawa wa Ujerumani waliokuwa kwenye utawala wa Hitler wakisema walisababisha vifo vingi vya raia wa Marekani na washirika wake kwenye vita vya pili vya dunia. Ila kwa serikali ya Marekani, waliona kuna mafaa mengi kwa usalama wa taifa hilo katika kuwa na mainjinia hawa huru na kufanya kazi kwa niaba ya shirika la NASA na kitengo cha roketi kwa matumizi ya kijeshi.
No Comment! Be the first one.