fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

simu Teknolojia

NOKIA: Display Kubwa Ni ‘Ujinga Tuu?’ Au Teknolojia Ndio Ina Tija Zaidi?

NOKIA: Display Kubwa Ni ‘Ujinga Tuu?’ Au Teknolojia Ndio Ina Tija Zaidi?

Kwa sasa simu janja zipo katika ukubwa wa aina tofauti tofauti. Je, ukubwa wa simu janja una tija kweli au sio kitu cha msingi kama vile kampuni nguli la Nokia linavyosema?

Pengine kwa wengine umbo ni kitu cha muhimu zaidi katika simu. Vipi kuhusu na teknolojia ya ndani ya simu hiyo lakini? Ni jambo la msingi kuwa na teknolojia kubwa ndani ya simu hilo liko wazi.

Ukubwa Wa Kioo Cha SImu

Ukubwa Wa Kioo Cha SImu

Kwani umbo ni kitu cha muhimu sana au tunafuata mikumbo tuu? Pengine simu yenye kioo (display) kubwa sio ujinga bali ni matakwa ya mtu. Watu tuna machaguo sio? Pengine matumizi yako na yangu yako ni tofauti.

Mtu unaweza pendelea kutumia simu yenye kioo ndogo kwa sababu labda mahitaji mambo mengi katika simu. Fikiria mtu ambae ana matumizi mengi katika simu kama vile  kutazama picha jongefu, kucheza magemu, kutuma barua pepe na mambo mengine mengi ambayo yanaladhimu kuwa na simu yenye kioo kikubwa.

Simu janja

Simu ndogo kwa upande mwengine sio kitu kibaya sana kuwa nacho haswa kwa wale wanaopenda simu ambazo zinakaa vizuri katika mkono. ukiachana na hilo ni kwamba simu janja ndogo ni kwamba kwa kawaida haziwezi kuwa na vipengele vingi ukilinganisha na simu kubwa.

SOMA PIA  Apple yapunguza bei ya betri ya simu zake

Kila mtu ana mawazo yake lakini katika kuangalia ni kifaa gani anakipenda na ana uwezo wa kukitumia, ningependa kuskia kutoka kwako wewe upo wapi kati kuchagua simu, je ungependa simu ndogo au kubwa? niandikie hapo chini katika sanduku la maoni.

Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Pendwa Wa TeknoKona Kila Siku Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!

Hashiman (@hashdough) Nuh

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi.
Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania