fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

apps instagram Intaneti

Instagram Live Rooms – Watu wanne kuweza kuwa katika mazungumzo kwa njia ya Video. #Live

Instagram Live Rooms – Watu wanne kuweza kuwa katika mazungumzo kwa njia ya Video. #Live

Instagram watambulisha Instagram Live Rooms, uwezo wa hadi watu wanne kufanya mazungumzo ya mubashara.

Kwa muda mrefu kulikuwa na uwezo wa watu wawili kwenda mubashara pamoja na kufanya mazungumzo kupitia Instagram Live.

instagram live rooms

Kupitia Instagram Live Rooms itakuwa rahisi kwa watu wanaotaka kufanya vipindi vya mfumo wa vipindi (show) zinazohusisha watu wengi kuweza kufanya hivyo kupitia Instagram kwa urahisi.

Ushindani dhidi ya Zoom na app ya Clubhouse

Zoom: Huduma ya Zoom ndio imekuwa moja ya huduma muhimu katika kuwezesha mazungumzo yenye wadau wengi. Instagram Live Room inaweza waibia watumiaji ambao huwa wanahitaji watazamaji wengi, na kwa washiriki mazungumzo wasiozidi wanne.

SOMA PIA  FourSquare Sasa Yawezesha Ku 'Check In' Marafiki !

Clubhouse: Clubhouse ni app inayokuja juu kwa kasi kwa sasa, bado inapatikana kwa watumiaji wa iPhone tuu. App hii inawezesha watu kadhaa kufanya mazungumzo yao, na kuwapa nafasi watu wengine wengi kuwa wasikilizaji wa mazungumzo hayo. Teknolojia inayotumika ni ya sauti tuu.

app ya clubhouse

Inasemekana tayari Facebook wanafanyia kazi app ya kuja kushindana na Clubhouse

Uzuri wa huduma hii ni kwamba yule aliyeanzisha mazungumzo hayo atapata kuwafikia hadi wanao’follow wageni wake wa kwenye mazungumzo. Followers wa washiriki watapata notification kuhusu video iliyoenda LIVE.

SOMA PIA  Kufuta Meseji WhatsApp: Sasa ni rasmi kwa watumiaji wa app hii maarufu

Tayari inasemekana Facebook wanatengeneza huduma nyingine kwa ajili ya kushindana moja kwa moja na app ya Clubhouse. Walichofanya kwenye kuleta Instagram Live Rooms ni mwanzo tuu, kwa muda mrefu Facebook amekuwa na sifa ya kuiga vitu kwa wengine kama wanashindwa kuwanunua – wamefanya hili kupitia ‘Stories’ waliposhindwa kuinunua Snapchat, walikuja na Reels waliposhindwa kuinunua TikTok.

SOMA PIA  WhatsApp kurudisha "status" za maneno..

Instagram Live Rooms itaweza kuchochea utumiaji zaidi wa video za mubashara. Kwa sasa wanaufanyia uwezo huo majaribio kwa watumiaji wachache wa iPhone, uwezo huo unategemewa kuwafikia watumiaji wengine wote ndani ya siku zichache zijazo. Endelea kusasisha (update) app yako ya Instagram na utapata taarifa ikianza kupatikana kwako.

Chanzo: Instagram

Comrade Mokiwa

Comrade Mokiwa

Muanzilishi wa Teknokona na Teknokona Group LTD - WWW.TEKNOKONAGROUP.COM

Muda wangu umegawanyika kati ya kazi kibunifu @teknokonagroup na uandishi wa habari za Teknolojia hapa Teknokona Blog.

| mhariri(at)teknokona.co.tz |

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania