Kufurahishwa huko kunatokana na ongezeko la matumizi ya magari yanayojiendesha yenyewe nchini humo ambapo serikali ya Marekani imechapisha maelezo ya kusimamia ongezeko la magari yanayojiendesha nchini humo.
Katika sera ya hivi karibuni kuhusiana na magari yanayojiendesha yenyewe imayojumuisha mambo 15 ndani yake imetoa angalizo kwa makampuni yanayojihusisha na utengenezaji wa gari hizo kuhakisha wanaangalia uwezo wa gari hizo kuweza kuhifadhi kumbukumbu na pia kuweza kumshirikisha na nweingine (share).
Katika chapisho la gazeti moja, rais Obama amesema kuwa magari yanayojiendesha yamepiga hatua ya kuwa hali halisi inayojitokeza baada ya kuonekana kuwa ndoto hapo awali. Kauli hiyo inajidhihirisha zaidi kwa Uber kuamua kutumia usafiri wa magari yanayojiendesha yenyewe. Soma zaidi HAPA.
Rais Obama anaamini kuwa magari hayo yanaweza kuokoa maisha ya wengi pamoja na wale wasioendesha magari kwa sasa na kuongeza kuwa ni lazima serikali iweke nguvu za ziada kuweza kuifikisha teknolojia hiyo mbali zaidi ingawa kabla ya yote ni muhimu serikali kutambua usalama wa mtuamiji awapo katika gari hiyo.
Usalama katika kila jambo ni kitu muhimu sana. Takwimu zinaonyesha kuwa takribani zaidi ya watu 35 elfu walikufa kwa mwaka jana kutokana na ajali za barabarani. Mwezi Juni dereva mmoja aliyekuwa akiendesha gari linalojiendesha lenyewe alipata ajali, unaweza kusoma zaidi.
Vyanzo: Business insider, BBC