Instagram ni moja ya mtandao wa kujamii unaotumiwa na watu wengi duniani na hata kuwa sehemu ya chanzo cha mapato. Hii inatokana na kwamba watu wengi wanatumia Instagram kwa mambo mengi tuu ikiwemo kufanya biashara kidijitali.
Unaweza usikubali kuwa una uraibu wa kutumia Instagram lakini hilo linawezekana kabisa. Ni wazi kuwa Na kwa mujibu wmatumizi yetu ya Instagram yanatokana na sababu mbalimbali. Kwa mujibu wa takwimu za Meta (Kampuni mama inayomiliki bidhaa zote zilizokuwa chini ya Facebook hapo awali) zinaonyesha taakribuni watu bilioni moja hutuma jumbe za biashara kwenye Instgram.
Katika hilo Instagram imeboreshwa ambapo sasa mtu anaweza akafanya manunuzi ya bidhaaa aliyoonyeshwa na muuzaji wakati wanabadilisha jumbe kwenye uwanja mahususi (chats). Fikiria mathalani wewe kama mteja mfanyabiashara kwa njia ya mtandao amekuonyesha fulana na ukavutuwa nayo basi mara baada ya pande pili kuafikiana mchakato wa kuwezesha biashara kufanyika utaanza mara moja.

Si tu uwezo wa kufanya malipo bali hapohapo unaweza ukamuuliza yule anayekuuzia kuhusiana na mzigo wakop umefikia wapi na hata kuweza kuufuatilia kama vile ambavyo tunaweza kufanya tukinunua vitu kutoka sehemu mbalimbali duniani. Na si kwa kutumia kadi yako ya benki tu bali mteja naweza kufanya malipo kupitia Meta Pay.
Haya sasa ule usemi wa “Dunia ni kijiji” unazidi kupaa kwani sasa watu wanaweza kununua kitu au vitu walivyopendezwa navyo kwenye Instagram kwa urahisi kabisa. Natumaini sasa umefahamu na kama ulikuwa hujui basi hakiksha unatumia toleo la karibuni kabisa ili kuweza kuona maboresho hayo.
Vyanzo: GSMArena, mitandao mbalimbali
No Comment! Be the first one.