fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Google simu Teknolojia

Project Ara: Simu za Kuchomeka chomeka vifaa (parts) kutoka Google zipo njiani

Project Ara: Simu za Kuchomeka chomeka vifaa (parts) kutoka Google zipo njiani

Spread the love

Tulishaandika kuhusu ujio wa simu janja za kuchochomeka ‘parts’ zake zinatengenezwa na Google, zikitambulika kwa jina la ‘Project Ara’. Sasa ni rasmi, zitegemee kupatikana mwaka 2017.

Simu janja Project Ara

Unamaanisha nini unaposema za kuchomechomeka parts?

Kwa kifupi ni simu janja ambazo ukinunua moja basi hautalazimika kutumia pesa nyingi kuiboresha vitu kama vile uwezo wa kamera, spika, RAM, au ata ujazo wa diski (storage). Vitu kama hivi vitakuwa vinaweza kuchomolewa kimoja kimoja na kupachika kingine.

Hii ina maanisha hakutakuwa na ulazima wa kutoa matoleo mengi ya simu inayofanana fanana uwezo. Una nunua msingi (kwa sisi hichi kina prosesa na ‘display’) kisha unaweza badili badili vitu vingine kila vinapoletwa.

Ujapenda uwezo wa kamera? Basi hauitaji kununua simu mpya, unanunua tuu kipande cha kamera chenye uwezo mkubwa zaidi na kukipachika kwenye simu yako.

Kupitia kongamano lao la Google I/O wiki iliyopita Google wameweza kuonesha simu hizo zikiwa zinafanya kazi vizuri tuu na kusema mpango wao upo pale pale. Na kwa simu hizi ni wao ndio watakaosimamia kila kitu, hii ni tofauti na simu zao za Nexus ambazo wao ufanya ubunifu na kisha zinatengenezwa na makampuni mengine kama vile HTC. Hizi watatengeneza na kuuza wenyewe.

Machache ya kufahamu kwa sasa

Project Ara

Ubunifu? Vipande pia vitaweza patikana vya rangi mbalimbali, hivyo utakuwa na uhuru katika ubunifu wa muonekano wa simu yako

> Iambie simu ‘Okay Google, eject the camera module’ na kipande cha kamera kitachomoka

Ndio, vipande vya kuunga unga vinaitwa ‘module’ kimombo, na kuvichomoa hautaitaji kutumia nguvu….utatumia maneno tuu, utaiambia simu ichomoe na itachomoa kipande husika na wewe utaweza kubadilisha na kuweka kingine. Fundi hataitajika, mabadiliko yataweza fanywa na mtumiaji mwenyewe.

SOMA PIA  Adele amkomesha aliyekuwa akimrekodi; Je alikuwa sahihi?

> Hadi betri ni la kuchomoa pia.

Simu hizi hazitakuwa nyembamba sana kama vile zingine nyingi kwa sasa zilivyo ambazo betri hazichomoki…utaweza pia kubadilisha uwezo wa betri kwa mfumo huo huo wa kuchomoa.

> Kwa sasa prosesa haichomoki ila ni kwa sasa tuu,

Ndio wamesema kwa sasa wameona ni vizuri ibakie ila baadae katika hayo matoleo rasmi yaliyo njiani kutoka na kuuzika utaweza ata kuchomoa na kubadilisha kipande chenye prosesa.

vipande simu project ara

Lengo ni kwamba ata watengenezaji wengine wa vifaa kama kamera, prosesa, betri n.k pia wajiingize kwenye utengenezaji wa vipande (modules) za simu hizi za project ara.

Simu hizi zitatumia Android. Na inasemekana zitaanza kupatikana kwa ajili ya watengenezaji apps na n.k (developers) muda si mrefu na mpango wao ni ziweze kuingia sokoni mwakani. Pia Google itakaribisha makampuni mengine pia kuweza kutengeneza parts (vipande) na kuziuza kivyao kwa ajili ya kutumika kwenye simu hizi.

SOMA PIA  Pata wasaha wa kuifahamu simu janja Samsung Galaxy A03s

Soma Pia – ACER kuja na kompyuta za muunganisho

Je una mtazamo gani juu ya teknolojia hii ya project Ara? Kwa mtazamo wetu ni kwamba itasaidia sana kuondoa hali ya sasa ambapo watu inawabidi kutoa pesa mingi kununua toleo jipya la simu lenye maboresho madogo tuu kutoka ile ambayo anatumia.

Comrade Mokiwa

Mbunifu na mpenda teknolojia.

Muanzilishi wa Teknokona, TechMsaada na Teknokona Group LTD - WWW.TEKNOKONAGROUP.COM

Muda wangu umegawanyika kati ya kazi kibunifu @teknokonagroup na uandishi wa habari za Teknolojia hapa Teknokona Blog.

| mhariri(at)teknokona.co.tz |

Comment

TeknoKona Teknolojia Tanzania