fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Google Intaneti

Google Drive: Pata GB 2 zaidi za Diski Uhifadhi katika Akaunti yako BURE!

Google Drive: Pata GB 2 zaidi za Diski Uhifadhi katika Akaunti yako BURE!

Spread the love

Katika maadhimisho wa siku salama ya huduma ya intaneti duniani – Safer Internet Day, mtandao wa Google unawapatia watumiaji wake GB 2 zaidi za diski uhifadhi bure kabisa katika huduma ya Google Drive.

Safer Internet Day ni kitu ambacho inawezekana hujawahi kukisikia kabla ya leo, hii ni siku maalumu iliyoanzishwa kukumbushia watu umuhimu wa kuhakikisha akaunti zao zipo salama.

drive-google-drive Google Drive

Katika kuhakikisha hilo linatokea Google wanawapa sababu za watu kuhakikisha wanapitia mipangilio (setting) za akaunti yao kuhakikisha kama mambo yote yapo sawa. NA MWISHO WANAKUPA ZAWADI YA GB 2 BURE KWENYE AKAUNTI YA GOOGLE DRIVE.

SOMA PIA  Facebook Wanakupa Uhuru wa Kuchagua Marafiki Wakuu

Promosheni ndio imeanza na inategemewa kuwepo kwa takribani wiki moja, inasemekana mwaka jana ilidumu kwa wiki moja.

Unaweza kwenda kuanza kuangalia taarifa muhimu za akaunti yako na kuhakikisha vitu kama vile sehemu ambazo akaunti yako ime-login n.k kupitia hapa -> Google Account Settings

SOMA PIA  Facebook yawezesha kutuma picha zenye ubora wa 4K kwenye Messenger

Pia unaweza tembelea mtandao wa Safe Internet Day – https://www.saferinternetday.org/ ili kufahamu zaidi kuhusu siku huu, inaonekana maadhimisho yameshafanyika kwa takribani miaka miwili kwa sasa.

Comrade Mokiwa

Mbunifu na mpenda teknolojia.

Muanzilishi wa Teknokona, TechMsaada na Teknokona Group LTD - WWW.TEKNOKONAGROUP.COM

Muda wangu umegawanyika kati ya kazi kibunifu @teknokonagroup na uandishi wa habari za Teknolojia hapa Teknokona Blog.

| mhariri(at)teknokona.co.tz |

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

TeknoKona Teknolojia Tanzania