fbpx
Android, apps, Intaneti, Mtandao wa Kijamii, simu

Twitter Lite yaanza kupatikana katika baaadhi ya nchi

twitter-lite-yaanza-kupatikana-katika-baaadhi-ya-nchi
Sambaza

Twitter Lite ikiwa na lengo la kuvutia watu na kuongeza idadi ya watu wanaotumia Twitter sasa inapatikana kupitia Google Play Store katika zaidi ya nchi 24 na Tanzania ikiwa miongoni mwa nchi hizo.

Kwa miezi kadhaa Twitter Lite imekuwa katika hatua ya majaribio na baada ya kupokea maoni mazuri kutoka kwa waliotumia app hiyo Twitter wakaamua kutanua wigo wa upatikanaji wa app hiyo, mtangulizi wake akiwa app kuu ya Twitter ambayo ndio ilizoeleka kutumiwa na wengi.

Nini maana ya neno ‘Lite‘ kwenye programu tumishi yoyote?

Maana ya neno “Lite” kwenye app yoyote (Facebook Lite, Twitter Lite, n.k) ni kwamba inatumia kiasi kidogo sana cha kifuruishi cha intaneti (MBs) kulinganisha na app kuu yenye jina sawa na hilo ila yenyewe haiishii na neno Lite.

Pia ina ukubwa mdogo kulinganisha na ukubwa wa app ambayo mtangulizi wake (inachukua nafasi ndogo kwenye memori).

Sifa za Twitter Lite.

>Kwanza kabisa Twitter Lite inapatikana kwa simu za Android tu hivi sasa na ukubwa wa app yenyewe hauzidi MB 3. App hiyo inachukua muda mfupi wa kufungua picha/video kutokana na kukubali teknolojia ya 2G pamoja na 3G,

INAYOHUSIANA  Bidhaa za Apple zitakazotoka Septemba-Oktoba 2020

>Unaweza kutumia bila ya MBs kutumika (ukiwa offline) pia inaruhusu kuchagua kufungua picha/video ambayo mtumiaji anataka kuiona kama ilivyo kwenye Facebook Lite,

Muonekano wa Twitter Lite: App mbadala wa app kuu ya Twitter. App hiyo inatumia kiasi kidogo cha intaneti.

>Inatumia kiasi kidogo cha intaneti na inafunguka kwa haraka sehemu ambayo mtandao uko chini sana.

Hivi sasa Twitter inapatikana Algeria, Bangladesh, Bolivia, Brazil, Chile, Colombia, Costa Rica, Ecuador, Misri, Israeli, Kazakhstan, Mexico, Malaysia, Nigeria, Nepal, Panama, Peru, Serbia, El Salvador, Afrika Kusini, Thailand, Tunisia, Tanzania, na Venezuela.

Upatikanaji rasmi wa app hiyo unatarajiwa kuongeza idadi ya watumiaji mtandao wa kijamii wa Twitter ambapo hivi sasa ina watumiaji milioni 330 wa kila mwezi na 80% kati ya hao wanatoka nje ya Marekani.

Android: Bofya>>Kupakua Twitter Lite

Vyanzo: Gadgets 360, Engadget

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Notice: Trying to access array offset on value of type null in /home/teknoloj/public_html/wp-content/plugins/intelly-related-posts/includes/core.php on line 163

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|