fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Kompyuta Teknolojia Windows 11

Muundo mpya wa muonekano wa tabiti kwenye Windows 11

Muundo mpya wa muonekano wa tabiti kwenye Windows 11

Spread the love

Windows 11 ni programu endeshi ambayo inawika sehemu nyingi duniani na inachagizwa na upya wake kitu ambacho watu wengi ulimwenguni wanaweka toleo hilo kwenye kompyuta zao bila kujali kifaa husika kimekidhi vigezo vya kuwa na sifa zinazohitajika kuwa katika sehemu salama ya kupakua masasisho yanapotoka.

Maboresho mbalimbali yamekuwa yakifanyika kwenye toleo hilo la programu endeshi tangu kutoka kwake rasmi mwanzoni mwa mwezi Oktoba mwaka jana, Bado tutazidi kuyafahamu mengi lakini hivi sasa umetoka muundo mpya wa mpangilio wa vitukwenye ile sura ya tabiti kwenye Windows 11.

SOMA PIA  Kuharibika kwa Setilaiti ya Facebook, Tanzania na Afrika zimekosa Fursa?

Katika maboresho ambayo yameletwa ni uwezo wa kuchaguakuonekana kwa vitu vingi au vichache kifaa kikiwa katika muundo wa muonekano wa tabiti; ule mstari wa chini kabisa kwenye sura ya mbele ya Windows 11 hivi sasa mtumiaji watoleo husika la programu endeshi anaweza kupanga vikaonekana vitu vichache tu mfano alama ya Bluetooth, intaneti (WiFi), n.k.

Uwezo wa kuchagua vitu gani vionekane kiurahisisha kufanya mipanglio muhimu.

Pia, katika muonekano huo wa tabiti kwenye Windows 11 inaonekana vionjo viongezeka hasa katika muonekano ambapo sasa mtu anaweza kubofya sehemu na kuona vitu vingi ambavyo vinakuwa na maelezo kuhusu habari fulani.

muonekano wa tabiti

Muonwkano wa Windows 11 katika muundo wa tabiti.

Halikadhalika, maboesho hayo yamekwenda sambamba na ujio wa vikatuni vipya ambavyo mtu anaweza kuvitumia kumaanisha kitu fulani katika mtindo wa lugha ya picha.muonekano wa tabiti

SOMA PIA  TikTok kufungiwa Marekani: Muda umesogezwa mpaka siku 90

Tukumbuke kuwa ili kuweza kuona maboresho hayo (mathalani muonekano wa tabiti kwenye Windows 11) ni lazima kuyapakua na daima ni muhimu kwani pamoja na mengineyo yanayoboreshwa ni kwa ajili ya kufanya kompyuta zetu ziwe na ulinzi madhubuti.

Vyanzo: GSMArena, mitandao mbalimbali

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

TeknoKona Teknolojia Tanzania