Mtandao wa SMART umedhidi kujiimarisha katika mkoa wa Dar es salaam kwa kuongeza idadi ya minara yake kwa ajili ya intaneti ya kasi ya 4G.
SMART wameongeza minara maeneo 7 zaidi hii ikiwa ni pamoja na Magomeni Makanya, Kigogo, Makongo na Mwananyamala kisiwani.
Ni dhahiri kwamba kama unaishi Dar es salaam na unataka huduma za mtandao wa 4G kwa ubora wa juu na katika gharama naafuu basi SMART ndio mtandao unaoutafuta. Ingawa ni kweli maeneo mengine bado hawajayafikia ila wanazidi kuongeza minara hii kwa kasi kushinda mitandao mingine yoote inayotoa 4G.
Kufikia mwisho wa mwaka 2015 mtandao wa Smart ulikuwa na minara 80 yenye uwezo wa teknolojia ya 4G LTE jijini Dar es Salaam, kuongeza hii saba mipya inapeleka idadi hiyo kufikia 87 hadi sasa.
Kwa mwezi mmoja sasa nimekuwa natumia mtandao huu (asante kwa udhamini wao ) na kwakweli nilishangazwa na speed ya mtandao huu nilijaribu kurekodi mara kwa mara na kunawakati niliweza kupata hadi 10.82 Mbps kwa ku download huku niki upload kwa 4.42 Mbps. Hii ni speed ambayo mitandao mingi haiwezi kuifikia ingawa wamekuwa wakijitangaza kuwa wanakasi kubwa.
SMART wamejidhatiti katika mkoa wa Dar es salaam katika maeneo mengi zaidi ya mitandao mingi mikubwa ambayo inatoa huduma hii ya intaneti ya kasi ya 4G kwa maeneo machache. Kwa maneno mafupi ni kwamba SMART wanaongeza minara kwa kasi ndogo huku wakifikia maeneo mengi ambayo mitandao mingine bado haijafika.
Kama wewe ni mkazi wa Dar es salaam na unataka intanet yenye kasi ya 4G ya uhakika na inayopatikana maeneo mengi zaidi na kwa bei ya unafaa basi mtandao wa Smart unaweza ukawa ni chaguo bora zaidi.
No Comment! Be the first one.