ASUS? Ndiyo, kampuni mashuhuri katika utengenezaji wa laptop inakuja na simu janja yenye sifa kali sana katika uwezo wa kamera – ZenFone Zoom. Na hili limewezeshwa kupitia ushirikiano na mzuri na kampuni ya Panasonic na HOYA.
Panasonic ndio waliotengeneza ‘sensor’ spesheli ya Megapixel 13 na kampuni ya HOYA ndio waliotengeneza lenzi (lens) 10 spesheli zilizokwenye kila simu hiyo. Teknolojia hizi mbili ndio zimeweza kufanya kamera hii kuwa bora zaidi katika sifa ya ‘optical zoom’, tena bila ata ya kuwa na mnundu mkubwa eneo la kamera.
‘Optical Zoom’ – ndio sifa kuu ya kamera ya kisasa ya digitali yenye uwezo halisia wa kuwezesha kuchukua picha za umbali mkubwa kuonekana kwenye picha kwa ukaribu zaidi.
Katika kamera za simu mara nyingi simu zina ‘digital zoom’ na si ‘optical zoom’, digital zoom kiuhalisia kuna kuwa hakuna lens zozote zinazojisogeza kwenye kamera kuweza ku’zoom’ bali kinachofanyika ni kamera yako kukata eneo lile linalopazunguka pale unapotaka kupapiga picha.
Hii inafanya ubora wa picha yaani ‘quality’ kupungua. Ili kuwa na uwezo halisi wa optical zoom lazima kuwe na lens zinazosogea na kujirudisha pale unapozoom ili kuhakikisha unaendelea kuwa na picha ya ‘quality’ nzuri ata pale unapozoom.
Simu ya ZenFone Zoom ishaanza kupewa sifa ya kuwa ndio simu nyembamba zaidi duniani inayotumia teknolojia ya Optical Zoom.
Pia simu hii inakuja na kamera ya selfi ya Megapixel 5.
Sifa zingine za simu ya ZenFone Zoom;
- Laini moja, (Micro SIM)
- Kioo (display) chake ni cha teknolojia ngumu ya Gorilla Glass toleo la 4. Ni cha ukubwa wa inchi 5.5 na kiwango cha HD cha 1080p
- Prosesa – Atom quad-core processor (Z3950, up to 2.5GHz), a PowerVR G6430 GPU,
- RAM ya 4GB
- Diski uhifadhi (Storage) – GB 64, pia inakuja na uwezo wa kutumia memori kadi (MicroSD) ya ukubwa wa hadi GB 128
- Betri ni la mAh 3,000 na si la kuchomoa.
Programu endeshaji – Android 5.0 inayotumia muonekano unaotambulika kama ASUS ZenUI
Bodi ya simu hii ni ya alumini ila kwa nyuma ina kava la ngozi linalofunguka kwa ajili ya eneo la laini na memori kadi.
ASUS wanadai kazi nzito ya ubunifu na utengenezaji wa simu ya ZenFone Zoom imechukua miaka miwili na kuna ata vipindi kadhaa ambapo bado nusu waachane na mpango wa kuitengeneza.
Bei? – Nchini Marekani inategemewa kuuzwa kwa takribani dola 339 za nchini humo, ambayo ni takribani Tsh 875,000/= au Ksh 40,800/=.
Simu hiyo itaanza kupatikana nchini India mwishoni wa mwezi huu, Marekani na masoko mengine kuanzia mwezi ujao.
Je wewe ni mpenda picha za ubora wa hali ya juu? Basi simu ya ZenFone Zoom inaweza kukufaa.
Tuambie maoni yako, na kumbuka kusambaza makala kwa marafiki kupitia WhatsApp, Twitter, Facebook n.k.
Picha na Pulse.com, PcMag.com na mitandao mingine.
No Comment! Be the first one.