fbpx

Miwani kwa ajili ya watu wafupi kuweza kuona mbali

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Uwezo wa kuona mbali kwa wengine ni changamoto kutokana na vimo vyao lakini teknolojia inakua kila leo vilevile inaaangazia kila pembe ambapo leo utafahamu ubunifu uliolenga moja kwa moja kundi fulani la watu.

Katika pitapita zangu nikakutana kitu cha kupendeza hasa kwa yeyote ambae anajali na kuguswa kutokana na kile ambacho mtu mwingine anakipitia na baada ya kumaliza kusoma makala hii naamini itakuwa imewafurahisha wengi.

Kwenye halaiki ya watu watu ambao si warefu wanapata wakati mgumu kuweza kutazama vitu vilivyo mbali na mboni za macho yao kutokana na jinsi walivyo. Sasa unaweza ukacheka lakini ukweli ni kwamba watu hawa teknolojia ya leo imeondoa ile adha ya wao kupata tabu ya kuona kilw ambacho hawawezi kukiona kirahisi.

INAYOHUSIANA  OralQuick: Upo Tayari Kujipima Ukimwi?

Fahamu miwani inayoafaa watu wafupi.

Mbunifu, Bw. Dominic Wilcox ametegeneza miwani inayowawezesha watu ambao si warefu kuweza kuona kinachoendelea mbele kutokana na upeo wa macho yao kutoruhusu kwa sababu mbalimbali. Nitaeleweka vizuri nikitumia mfano huu: Umekwenda kwenye tamasha fulani na mwenza/mtoto wako lakini ili na yeye aweze kupata uhondo wa kile kinachoendelea tofauti na kusikia shangwe za watu/muziki inakulazimu umbebe na akae kwenye mabega yako, si ndio?.

INAYOHUSIANA  Toshiba T1100 - Ifahamu Laptop ya Kwanza Kuweza Nunuliwa na Mtu Yeyote Duniani

Miwani hiyo inaitwa “One foot taller” ambayo inamuwezesha mtumiaji kuweza kuona kitu kilicho umbali wa karibu sentimita 30.5 zaidi kuliko uwezo wa macho yetu, inayowasaidia watu warefu kutokuwa kikwazo kwa wengine kutokana na walivyoumbwa (kuwa warefu) hivyo basi kufanya wale ambao wamewazidi urefu kushindwa kuoma kilicho mbele yao kwa mbali.

watu wafupi

“Wazo la kutengeneza miwani ya ina hiyo lilikuja baada kwenda kwenye ukumbi wa starehe ambapo bendi moja ya muziki ilikuwa inatumbwiza kisha nikamuona mwanamke mmoja akicheza muziki lakini anashindwa kuwaona wahusika (wanaotumbwiza)”~Dominic Wilcox.

Lenzi za kwenye miwani hiyo zimetengenezwa kwa teknolojia moja ambapo ili ndogo imefunwa kwenye pembe ya nyuzi 45 na kile kikubwa kimewekwa kwa kupitisha kidogo usawa wa macho ya mvaaaji hivyo kuweza kutekeleza kile ambacho kimekusudiwa.

watu wafupi

Muonekano wa “One foot taller” kwa karibu liyotengezwa kutokana na watu wafupi kupata shida fulani wakati wanapotaka kuona kitu kilicho mbali nao.

Haya sasa wewe msomaji wetu ni miongoni mwa wale ambao wanakumbana na changamoto ya kujua kinachoendelea unapokwenda kwenye sehemu zenye mkusanyiko mkuwa wa watu?. Kwa hakika utakuwa umefurahi, tuambie maoni yako hapo chini.

Vyanzo: De Zeen, Mirror

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.