Microsoft waitaka Netflix mazima. Microsoft ni moja kati ya makampuni makubwa ambayo mara kwa mara yamekua yakiyanunua makampuni mengine mengi na kuwa chini yake.
Kitu kimoja ambacho kiko wazi tena kipo kwa makampuni haya mawili (Microsoft na Netflix) ni kwamba wote wawili wanajiwekeza zaidi katika maswala mazima ya magemu.
Tayari Microsoft wana uhusiano mzuri wa kibiashara na Netflix, kupitia mifumo ya kimatangazo. Maeneo ambayo tayari huduma ya Netflix ya bei nafuu inayokuja na matangazo inafanya kazi – teknolojia ya matangazo hayo ni ya Microsoft.
Wote wawili vitu ambavyo wanavifanya ili kubobea katika magemu vinaonekana, mfano Netflix ilinunua makampuni kadhaa ambayo yamejikita na uandaaji wa magemu huku Microsoft na yenyewe ikifanya hivyo.
Vyanzo kwa sasa vinasema tuu kuwa mkurugenzi mkuu wa Microsoft bwana Satya Nadella ana hilo wazo tuu na pengine anaweza akaliweka kata orodha ya makampuni ambayo wanaweza wakayanunua.
Mwanzoni kabisa kampuni iliweka orodha ya vitu na makampuni 273 ambayo walikua na mpango wa kuyanunua lakini baadae Mircosoft ikaanza kwanza na makampuni makubwa makubwa baada ya bwana Satya kupata cheo hicho.
Kumbuka kwa haraka haraka kampuni ilinunua makampuni haya kwa gharama kubwa sana:-
Waandaaji wa gemu ya Minecraft ambao ni Mojang studio walinunuliwa kwa bilioni $2.5 (2014); LinkedIn ilinunuliwa kwa bilioni $26 (2016).
GitHub studio walinunuliwa kwa bilioni $7.5 (2018); ZeniMax Media studio walinunuliwa kwa bilioni $8.1 (2020); Nuance Communications studio walinunuliwa kwa bilioni $19.7 (2021).
Huku Activision Blizzard studio nao walinunuliwa kwa bilioni $68.7 japokua dili hilo bado lina maswali mengi kwa wadau na linafanyiwa uchunguzi.
Hii inaonyesha dhahiri kwamba Microsoft wao hawashindwi kuinunua Netflix na kama wakifanya hivyo itawafanya kuingia rasmi na kubobea katika maonesho ya filamu na michizo ya kuigiza na mambo mengine mengi.
Huduma za Ku’stream kwa sasa zinaingiza mapato mengi huku zikiwa zinakua kwa kasi sana na zinaua njia za kawaida kama TV na Redio, pengine Microsoft nao wanataka kipande kidogo cha mkate kupitia huduma hizi.
Kingine ni kwamba makampuni haya yameshwahi kufanya kazi kwa pamoja kwa ukaribu wa hali ya juu, unakumbuka tuliandika kuhusu Microsift kuwa ndio msimamizi vifurushi vya bei rahisi ila venye matangazo
SOMA ZAIDI >>HAPA<<
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika eneo la comment je unadhani dili hili litafanikiwa kweli? Na je likifanikiwa unahisi litakua la bei gani kwa haraka haraka
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.