Unakumbuka tuliandika kuhusu kampuni ya Netflix kuanzisha mfumo wa matangazo mwaka huu? Kama Ulipitwa soma >>HAPA<<
Kinachofanyika hapa ni kwamba Netflix inapunguza bei katika vifurushi vyake lakini kutokana na kwamba bei hizo ni za chini basi mtumaiji wa huduma hiyo atakaua akipata matangazo wakati anaangalia video za humo ndani.
Miezi kadhaa iliyopita Netflix walikua wanatafuta kampuni ambayo wanaweza ingia nayo mikataba katika kuliwezesha hili na makampuni mengi yalikua kwenye mazungumzo.
Kwa taarifa ambayo imetolewa na kampuni ni kwamba kampuni ya Microsoft ndio imechaguliwa kuwa kampuni ambayo Netflix imeona inafaa na hivyo basi kuipa kazi ya matangazo.
Microsoft inakua ndio kampuni itakayo simamia matangazo na mshirika wake katika mauzo (global advertising technology and sales partner).
Microsoft wameonyesha thabiti kuwa na uwezo wa kukidhi haja zetu zote za kimatangazo huku tukiwa tunafanya kazi pamoja katika kuhakikisha kuwa huduma yetu mpya ya matangazo ndani ya Netflix inafanikiwa” —Netflix
Kingine kizuri ni kwamba kampuni hiyo ya Microsoft imeonyesha mpaka nia ya kuhusika mpaka kwenye mauzo, yaani haikuishia kwenye matangazo tuu vile vile bila kusahau kipengele cha ulinzi, usalama na usiri wa wateja.
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika eneo la comment, je hii umeipokeaje? Je unaweza ukawa unatumia huduma hii yenye matangazo?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.