fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Dell Tablet Tablets

Microsoft Kushirikiana Na Dell Pamoja Na HP Ili Kuuza Tabiti Zao Za Surface Pro!

Microsoft Kushirikiana Na Dell Pamoja Na HP Ili Kuuza Tabiti Zao Za Surface Pro!

Spread the love

Microsoft imejikita katika kuingia katika makubaliano ili kupata ushirikiano wa Dell pamoja na hewlett packard (HP) katika kuuza tabiti zake zinazojulikana kama Surface Pro kwa wateja wakubwa (makampuni).

Katika makubaliano hayo kampuni la dell litatumia kitengo chake cha mauzo, kuuza tabiti hizo za microsoft na vifaa kuanzia mwezi oktoba. Pia itawezekana hata kwa biashara hizo kununua tabiti za surface pro katika mtandao wa dell.

surface-pro-3-1940x1302

Tabiti Ya Microsoft ‘Surface Pro 3’

Habari hizi zinakuja baada ya soko la tabiti kuonyesha kushuka. kila mtu anaangalia atafanikiwa vipi kupata mauzo makubwa ya tabiti. Hata Apple wamefanya maboresho makubwa ya tabiti zao (iPad) ili mradi tuu wapate mauzo yanayoridhisha. Japokuwa microsoft ilipata mauzo makubwa tuu katika kuuza tabiti zao lakini bado wanataka kupata zaidi

Dhumuni kubwa la microfort ni kwamba lini malengo ya kupata zaidi (faida) kupitia makampuni makubwa ambayo yatanunua tabiti hizo kwa wingi na kwa pamoja . Lakini pengine labda kampuni hili linafanya hivi baada ya kusikia kuwa Apple wapo mzigoni kuja na iPad mpya

microsoft-surface-pro

Tabiti Ya Microsoft ‘Surface Pro’

Kampuni la microsoft sio la kwanza kuingia katika makubaliano na kampuni lingine kwa lengo la kuuziwa tabiti zake. Kampuni ya Apple na yenyewe iliingia mkataba mwezi agosti na kampuni ya CISCO  ili iuzie tabiti zake kwa biashara kubwa (makampuni). Licha ya hivyo pia kampuni imeingia mkataba na kampuni la IBM ikiwa na lengo kampuni hiyo (IBM) iwatemgemezee Apps zitakazo tumika katika biashara (Kama vile kwa makampuni)

SOMA PIA  Dell Precision 7730, Moja ya Laptop ya kiwango cha juu kutolewa na Dell. #2018

Maelezo kuhusiana na ushirikiano wa microsoft na Hewlett Packard bado haujawa wazi, lakini unaweza kushangaa ukawa kama ule ule unaofanana na Dell tuu.

Tuambie uamuzi huu unauchukuliaje? je unaonyesha kwamba microsoft labda imeelemewa mpaka haiwezi kuendesha soko lake? tuandikie sehemu ya comment. Tembelea mtandao wako pendwa wa TeknoKonaDotCom kila siku. TeknoKona Tupo Nawe Katika Teknolojia.

Hashiman (@hashdough) Nuh

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi.
Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

TeknoKona Teknolojia Tanzania