Lenovo imekuwa ni kampuni inajihusisha na masuala ya utengenezaji wa vifaa vya kiteknolojia kwa miaka sasa. Tukizungumzia kompyuta za mpakato au hata simu janja wengi watakuwa wanazifahamu/wameshawahi kuzitumia.
HIvi karibuni Lenovo wameamua kuishangaza dunia kwa kutoa tabiti (Tablet) za kutoka familia moja, yaani Tabiti 4 nne kwa mara moja. Jambo ambalo limeonekana kama ni njia mojawapo ya kuwafikia wale wateja wenye uwezo wa kununua bidhaa ambayo si ghali au zile ambzo ni ghali.
Katika onyesho lililohusisha vifaa mbalimbali lililoitwa MWC 2017 na kufanyika huko Barcelona mwezi Agosti kampuni mbalimbali ikiwemo Lenovo zilionnyesha bidhaa zao kwa mara ya kwaza. Lenovo ilitambulisha Tabiti zifuatazo:-
1. Lenovo Tab 4 8
- Kioo chake kina ukuwa wa inchi 8 na ubora wa 1280 x 800 pixels
- Ina prosesa ya Qualcomm Snapdragon 425 (prosesa 2 ndani ya 1)
- Diski ujazo wa 16GB
- RAM yake ina ukubwa wa 2GB
- Kamera ya nyuma ikiwa na 5MP na ile ya mbele (mahususi kwa selfie) ina 2MP
Tabiti Lenovo 4 8ndio nyenye uwezo wa kawaida kabisa na ni dhahiri kabisa hata bei yake si kubwa.
2. Lenovo Tab 4 8 Plus
- Kioo chake kina ukuwa inchi 8 na kuonyesha picha zenye muonekano wa hali ya juu (Full HD)
- Prosesa ni Qualcomm Snapdragon 625 (prosesa 8 ndani ya 1)
- Diski ujazo wa mpaka 64GB
- RAM yake ina ukubwa wa mpaka 4GB
- Kamera ya nyuma ina 8MP huku ile ya mbele ikiwa na 5MP
- Betri lake lina 4,850 mAh
- Ina teknolojia ya kutumia alama ya kidole
3. Lenovo Tab 4 10
- Kioo chake kina ukuwa wa inchi10.1 na ubora wa 1280 x 800 pixels
- Ina prosesa ya Qualcomm Snapdragon 425 (prosesa 2 ndani ya 1)
- Diski ujazo wa 16GB
- RAM yake ina ukubwa wa 2GB
- Kamera ya nyuma ikiwa na 8MP na ile ya mbele ikiwa na 5MP
- Ina teknolojia ya kutumia alama ya kidole
Lenovo Tab 4 10
4. Lenovo Tab 4 10 Plus
- Kioo chake kina ukuwa wa inchi 10.1-inch na kuonyesha picha zenye muonekano wa hali ya juu (Full HD)
- Prosesa ni Qualcomm Snapdragon 625 (prosesa 8 ndani ya 1)
- Diski ujazo wa mpaka 64GB
- RAM yake ina ukubwa wa mpaka 4GB
- Kamera ya nyuma ikiwa na 8MP na ile ya mbele ikiwa na 5MP
- Betri lake lina 7,000 mAh
- Ina spika mbili za mbele
- Ina teknolojia ya kutumia alama ya kidole
- Bei yake ni kuanzia $279 (Tsh. 626,355)
Lenovo 5 10 Plus ndio yenye uwezo wa hali ya juu kulinganisha na nyinginezo. Ina teknolojia ya USB-C.
Lenovo wametambulisha tabiti nne lakini hawakuweka wazi zitauzwa kiasi gani ila kiujumla bei yake itakuwa si ya kutisha. Tutawafahamisha pindi bei zake zitakawekwa wazi. Unauzungumziaje uzinduzi wa tabiti hizo kutoka Lenovo?
Vyanzo: The Verge, Lenovo