Kampuni ya Dell imetambulisha laptop inayokwenda kwa jina la Dell Precision 7730 Mobile Workstation Developer Edition.
Laptop hii inayokuja na programu endeshaji (OS) ya Windows 10 au Ubuntu Linux 16.04 inawalenga watumiaji wanaoitaji laptop inayobebeka na huku ikiwa bado na uwezo mkubwa wa ufanisi.
Laptop hii inawalenga zaidi watu wanaohitaji kompyuta yenye ufanisi wa juu lakini pia ikiwa na sifa ya kubebeka kwa urahisi.
Sifa za Dell Precision 7730 Mobile Workstation Developer Edition ni kama hivi;
- Intel Core Xeon E-2186M 6 -Core CPU
- Nvidia Quadro P5200 ikija na GB 16 za GPU.
- RAM ya GB 64 DDR4 2,400MHz (kupitia oda spesheli, unaweza kuongeza kiwango cha RAM hadi kufikia GB 128)
- Diski uhifadhi ni wa TB 2
- Display ni ya ukubwa wa inchi 17.3

Pia inakuja na USB 3.1, eneo la kadi ya SD, mfumo wa HDMI na Mini DisplayPort. Mfumo wa kuchaji wa Thunderbold 3 Type C.
Bei?
Laptop hii inapatikana kwa bei ya juu na hivyo ni watu wachache sana wanaweza kuimiliki. Inaonekana inafaa zaidi kwa watengenezaji wa programu za kompyuta na wengine walio kwenye kazi kama hizo, kwani ufanisi wake wa juu unakuja kwa bei ya juu pia. Dola 11,500 za Kimarekani, hii takribani Tsh Milioni 26 kwa sasa.