Ujio wa simu janja umeweza kubadilisha uharaka na unafuu kwa wengi wetu kwa kuzingatia kuwa hapo awali tulikuwa tukitumia muda mrefu kuandika chochote kwa simu. Mfano muda mwingine kuandika herufi moja ilikuwa inakubidi kubonyeza sehemu mara tatu hadi nne.
Sababu za kuchukua muda mrefu kuandika zilikuwa nyingi ikiwa ni pamoja na baadhi ya simu kuwa na buttons (vibonyezo vya keyboard) vigumu na kumfanya mtumiaji atumie muda mrefu kuandika sms na hata kumsababishia maumivu ya vidole baada ya kuituma sms hiyo.
Kwa miaka kadhaa hivi kampuni mbalimbali zimejaribu kuja na aina mbalimbali za simu janja na kufanya simu hizo kufanana “Features” lakini kutofautiana muundo wa simu/uwezo wa simu yenyewe. Mfano hai ni pale kampuni iitwayo Apple inajaribu kuongeza nakshi kwenye simu janja inazotengeneza yenye “3D Touch” kwenye touchscreen.
Na sasa timu ya watafiti kutoka Microsoft iko mbioni kuja na teknolojia mpya kwenye simu janja ambayo itakuwa na uwezo wa kuotea mahali ambapo atumiaji anataka kubonyeza kwenye hiyo simu janja ambayo haitakuwa na ulazima wa kugusa kioo chake(touchscreen) ili kuweza kubonyeza mahali fulani.
Aidha, simu janja hiyo itaweza pia kuotea sehemu utakayotaka kubonyeza kulingana na jinsi ambavyo utakuwa umeishika na wapi vidole vyako vitakuwa kwa wakati huo bila kushika kioo cha simu janja.
Ingawa Microsoft kutokuwa kampuni ya kwanza kuja na teknolojia hiyo, ikumbukwe kuwa kampuni ya Microsoft siyo ya kwanza kuja na teknolojia kama hii, kampuni ya Samsung inatumia teknolojia kama hiyo kwenye simu za Galaxy Note kupitia teknolojia ya Stylus.
Halikadhalika, Sony nao walikuja na teknolojia inayofanana na hiyo mwaka 2012 ingawa teknolojia hiyo iliwekwa kwenye toleo moja tu ya simu kwa sababu ilikuwa ina support baadhi ya apps zilizokuja nazo na iliitwa “Sony’s Floating Touch”.
Kuna aina mbili ya “Capacitive sensors” za touchscreens ambazo ni:
“The standard mutual capacitance sensors”-hii ni aina ya sensor ambayo imezoeleka kutumika kwenye aina mabimbali ya touchscreens.
Aina ya pili ni self-capacitance sensors ambazo Microsoft imepanga kutumia kwenye hiyo teknolojia mpya itakayokuja nayo.
Aina hii ya sensors ina uwezo mkubwa wa kuhisi wapi kidole chako kinataka kubonyeza, hapo awaliaina ya sensors ilikuwa na uwezo wa kutambua aina moja tu ya input (“single input”) lakini Microsoft ililiona hilo na kulipatia ufumbuzi ambapo haitakuwa ikitambua aina moja ya input bali aina tofauti tofauti za input.
Je una mtazamo gani juu ya ujio wa teknolojia hii? Niambie kupitia eneo la comment!