Uwezo wa kupiga simu za video upo njiani kuletwa katika app ya WhatsApp. Inaonekana kwa bahati mbaya uwezo huo ulionekana kwa muda kwa wale wanaotumia toleo la matengenezo la WhatsApp (WhatsApp beta).
Tayari WhatsApp ni app mashuhuri zaidi ya mawasiliano kwa sasa, inawatumiaji zaidi ya bilioni moja kila mwezi na ujio wa uwezo huo wa kupiga simu za kuonana (WhatsApp video call) basi app hii itazidi kujizatiti kuwa kama app muhimu zaidi ya mawasiliano.
Ni hivi karibuni tuu WhatsApp walileta uwezo wa kutumiana mafaili ya mfumo documents – PDF n.k, na pia wakaleta app yao kwenye kompyuta kupitia programu spesheli za kupakuliwa kwenye kompyuta za Windows na Mac, ni ukweli usiopingika ya kwamba kuongezwa kwa uwezo wa Videos Calls utaifanya app hiyo kumamilika mara dufu.
Skype – ipo hatarini kuanza kuibiwa watumiaji wake ata wale wa kiofisi. Kwani WhatsApp tayari inatumiwa na watumiaji wengi sana na hivyo kama wakileta uwezo wa hadi wa kupiga simu za video za kimakundi basi hakika Skype watajikuta katika hali ngumu kiushindani.