Kampuni ya Facebook mwezi huu imetangaza programu mpya iitwayo Mentions. Programu hii ni kwa watu maarufu wanaojulikana na mtandao wa facebook. Mtu anayejulikana na mtandao wa Facebook huwa na tiki ya bluu, kwenye profile yake ya facebook.
Programu hiyo ni kwa ajili ya mfumo wa simu za mikononi wa i-phone, yani mfumo wa IOS. Mtu yeyote wa kawaida anaweza kuweka programu hiyo kwneye simu yake ila tu hatoweza kuitumia. Pamoja na kuwaweka watu maarufu kando kama VIP, Mentions imetegnenzwa kuwasaidia watu maarufu kama Flaviana Matata, kuweza kusoma maoni ya watu wanaomfuatilia kwenye facebook na kuweza kuwajibu moja-kwa-moja kiurahisi zaidi. Programu hii inaonekana kama twitter kidogo ili kumudu gumzo la watu hao maarufu. Pia inaweza kutumika kuendesha mazungumzo ya kumuuliza mmarufu maswali ya papo kwa hapo amabayo kwa lugha ya kigeni yanajulikana kama Question and Answer sessions (Q & A).
Msemaji mmoja wa Facebook amekaririwa na mtandao maaarufu wa Mashable kuwa kutokana na Mentions, watu maarufu wameonekana kutumia Facebook kwa sasa mara mbili zaidi ya walivyokuwa wakitumia siku za nyuma. Kwa kutumia Mentions, watu maarufu wanasukumwa kuwashirikisha mashabiki wao kwa picha na video ili kuonyesha maisha, kazi na mafanikio yao. Hata hivyo, Facebook wameamua kubana programu hiyo isitumike na makampuni maafuru na inawezekana siku za karibuni ikafunguliwa kwa watu wa kawaida. Kwa sasa, kuitumia Mentions, hauna budi ‘kujiweka’ na kuwa mtu maarufu.
Kuhusu mchakato wa kujulikana na Facebook, kampuni inatambua watu wachache duniani wanaofahamika na pia inawatambua moja-kwa-moja watu au kurasa yenye wafuatiliaji (‘followers’) wengi sana.
Je, wewe ni mtu maarufu au unamjua mtu kama huyo anayeitumia Mentions? Tuashirikishe hapa au kwenye kurasa yetu ya facebook www.facebook.com/teknokona.
No Comment! Be the first one.