Wakati mapigano yakiaendelea huko Gaza kati ya majeshi ya Israeli na wanamgambo wa Hamas, watumiaji wa mitandao ya jamii nao hawako nyuma kuonyesha hisia zao.
Kuanzia July 10, kundi la kimataifa la StandWithUs liliwaomba watu watume picha kuonyesha ushirikiano wao na Israeli dhidi ya Hamas. Mpaka sasa wamepata takribani picha 1000 na zinaendelea kila siku kutoka wapalestina waisraeli wanaogopa yanayotokea huko Gaza.
Nao wanaosimamia msimamo wa Palestine hawako nyuma kurusha msimamo wao wakitumia #IStandWithPalestine kwenye Instagram kutuma picha za passport na maneno ya @IStandWith Palestine kwenye mikono yao. Picha hizo zimefikia takribani 4,000.
Mitandao ya jamii inaonekana kutumiwa na watu wengi kuonyesha muamko wao na jinsi wanavyojisikia kuhusu masahaiba yanaoendelea duniani. Wengine hatahivyo wanashangaa jinsi gani mtu anaweza kukimbia mabomu huku akipiga picha za mdabiko ama ‘selfie’ kwa lugha ya kigeni.
Pamoja na ‘Hashtag’ hizo, nyingine zinazotumika kufuatilia mapambano ya Gaza ni #prayforgaza, #gazaunderattack na kurasa ya facebook iitwayo I love IDF. Watu katika majiji mbalimbali duniani wanaendelea kuonyesha hisia zao pia kwa maandamano kama tulivyojionea hapa jijini DAr es Salaam, Tanzania wiki iliyopita kulaani mauaji ya Wapalestina huko Gaza.
Una chochote cha kuongezea kwenye sakata hili?
No Comment! Be the first one.