Kutokana na gazeti la New York Times, timu ya watu wa kampuni maarufu ya teknolojia, Google Nairobi wameanzisha mfumo mpya wa malipo ya usafiri nchini humo. Mfumo huo unajulikana kwa kadi maalmu yake ya malipo iitwayo BebaPay Card, ambayo ni bure kwa mtu yeyote mwenye akaunti ya Gmail. Kadi hiyo inaweza ‘ku-scaniwa’ na kondakta mweye simu ya Android. Wasafiri wanaweza kulipia BebaPay kwenye benki yoyote inayoshiriki mfumo huo mpya.
Inasemekana mfumo huo mpya utaweza kuwalinda wasafiri na mfumuko wa bei unaotokea mara nyingi kwa ubabe wa matatu. Mfumo huo utasaidia wamiliki wa matatu kudhibiti mahesabu ya nauli na pia serikali itapata uwezo mkubwa wa kukusanya mapato kutoka kwenye matatu hizo. Matumizi ya kadi hiyo yanatazamiwa kpunguza wizi na kumpa msafiri wa uhuru wa kusafiri bila kubeba pesa taslimu.
Pamoja na kusaidia serikali kukusanya mapato kirahisi, mfumo huo unaangaliwa kwa mtazamo mbaya na wamiliki wa matatu kwa sababu serikali itakuwa na dhamana ya kutoa cheki za malipo kwa wamiliki hao na si tena mfumo wa zamani ambapo mmiliki anapata fedha zake taslimu kutoka kwa madereva wao.
Wachambuzi kadhaa wameonyesha kuwa na wasiwasi na msimu huo, ikionekana kuwa mfumo huo umekuja kabla ya muda wake. Mfumo huu unakabiliwa na changamoto kadhaa ikiwemo wingi wa wamiliki wa matatu nchini Kenya na mfumo wa kulipia amabao umeelekea kwenye mabenki na siyo kwenye simu za mkononi amabapo kuna urahisi zaidi.
Serikali ya Kenya ilitoa ilani ya kuondoa matumizi ya fedha taslimu kwenye matatu kufikia Julai 1 ila jambo hilo limeonekana kufeli. Kwa sasa, juhudi zinafanyika kupeleka mfumo huo kwenye usafiri wa masbasi ya mkoani na kupeleka mfumo huo kwenye simu za mkononi.
Ni mfumo mzuri. Lakini changamoto ziangaliwe. Mfumo huu wa malipo unasaidia kuokoa muda, kupunguza adha ya kutembea na kiasi kingi cha fedha na kutafuta 'change'. Nashukuru kwa uchambuzi mzuri.