fbpx
Android, Google

Rasmi: Android O, sasa ni Android 8.0 Oreo :-)

rasmi-android-o-sasa-ni-android-8-0-oreo
Sambaza

Hatimaye Kampuni ya Google imefumbua fumbo la herufi O kwa toleo lake jipya la Android 8.0 kwamba herufi hiyo sasa inasimama jina la Oreo.

Tangazo la jina hilo lilitolewa katika jiji la New York muda mfupi baada ya kupatwa kwa jua katika nchi ya Marekani.

Android Oreo
Wananchi wakiangalia na kupiga picha Sanamu la Android Oreo lilowekwa nje ya makao makuu ya Google

Oreo ni aina ya Biskuti tamu za Chokoleti zinazozalishwa na kampuni kongwe ya kimarekani ya Nabisco (National Biscuit Company) yenye makao makuu yake huko East Hanover, New Jersey.

INAYOHUSIANA  Nile X: Simu janja ya kwanza kutengenezwa Misri yazinduliwa

Simu za kwanza kupata toleo la Oreo

Simu za Google Pixel, Nexus 5X na Nexus 6P zitakuwa simu za kwanza kupokea maboresho (Update) za toleo hilo la Android 8.0. Baadae zitafuatiwa na Pixel C na Nexus Player.

Hii ni mara ya pili kwa Google katika historia yake kushirikiana na kampuni ya vitafunio kwenye kuweka jina la toleo la Android. Toleo la kitkat(Version 4.4) lilikuwa na ushirikiano wa kibiashara na kampuni ya Nestle.

INAYOHUSIANA  Jinsi Ya Kuhifadhi Mafaili Yaliyoko Kwenye Simu/Kompyuta Katika Mtandao!

android oreo

Hata hivyo inaelezwa kwamba Google haikuilipa kampuni ya Nestle pesa yoyote kwa kutumia jina la Kitkat. Bali ulikuwa ushirikiano wa kirafiki uliotoa fursa kwa kila upande.

Toleo la Android Oreo linatarajiwa kuja na maboresho mengi ikiwemo na Emoj mpya zaidi ya 60, keyboard, kupunguza ulaji wa chaji ya Betri na mengine mengi.

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Siyan

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.