fbpx
Teknolojia, Windows 10

Mbwembwe zinazokuja kwenye Windows 10

mbwembwe-zinazokuja-kwenye-windows-10
Sambaza

Leo hii ukienda kununua kompyuta dukani kama haitakuwa imewekwa Windows 8 basi itakuwa na Windows 10 ambayo inaonekana kuwa na watumiaji wengi lakini sio wa kupindukia.

Tukiwa umebakiza zaidi ya mwezi mmoja kumaliza mwaka 2018 Microsoft wameweka bayana vitu ambavyo ameviboresha kwenye programu endeshi ya Windows. Na kiujumla vinaendana na teknolojia iliyopo ya leo/hivi karibuni:

>Muonekano murua wa uso wa mbele.

Katika ile hali ya kuifanya Windows 10 ivutie mara tu mtu atakapokuwa amefika kwenye uso wa mbele wahusika wameboresha kwa kuongeza muonekano mpya ambao unaweza kuchagua kuweka kwenye uso wa mbele. Muonekano huo una rangi ya Bluu bahari.

INAYOHUSIANA  Mabadiliko Twitter: Majina kutohesabika katika herufi 140
mbwembwe
Uso wa mbele mya kwenye Windows 10 katika masasisho yajayo.

>Kipengele cha muonekano wa giza.

Wataalam wa kutengeneza programu kupitia makampuni mbalimbali wanaongeza moja ya kipengele cha muonekano wa giza ambapo kimsingi kinasaidia mambo fulani fulani. Vivyo hivyo kwenye Windows 10 nayo imeongezwa kitu hicho ambapo utaweza kuchagua kuweka muonekano wa giza/kawaida kwenye kompyuta au kifaa kilicho na programu tumishi husika.

mbwembwe
Utaweza kuchagua kuweka muonakano wa giza/mwaga katoka mpangilio wa kimputa/programu tumishi.

Maboresho mengine ni kutoanzisha upya kompyuta bila mpangilio mara baada ya kumaliza kupakua masasisho lakini pia kile kipengele maarafu cha kunakili (snipping tool) nacho kinatakuwa na mbwembwe mpya.

Masasisho hayo yatatoka mwaka 2019 mwezi Aprili pamoja na maboresho mengine kwenye proramu endeshi husika.

Vyanzo: The Verge, TNW

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|