fbpx

Mark Zuckerberg wa Facebook aomba radhi kwa kashfa ya Analytica

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Hatimae mwanzilishi wa mtandao wa Facebook, Mark Zuckerberg kwa mara ya kwanza tangu kuzuka kwa kashfa ya Cambridge Analytica amevunja ukimya na kudai kwamba wamefanya makosa.

Analytica inatuhumiwa kuingilia data za watumiaji milioni 50 wa mtandao wa Facebook. Katika ujumbe wake kupitia ukurasa wake wa Facebook Zuckerberg amesema kitendo hicho kimewavunjia uaminifu. Hivyo, kutokana na hali hiyo ameahidi kufanyika mabadiliko kadhaa ili kutoingiliwa na kuibwa kwa taarifa za watumiaji wake.

aomba radhi kwa kashfa ya Analytica

Facebook imekuwa ikikumbwa na kashfa ya kuruhusu taarifa za watu wake kutumika bila kibali maalum katika miaka ya karibuni jambo ambalo limeitia doa kampuni hiyo na mauzo yake ya hisa kushuka sana katika kipindi kifupi.

“Tuna wajibu wa kuzilinda taarifa zenu, na kama tukishindwa kuzilinda hatuna sifa ya kuwahudumia, mimi ndiye niliyeanzisha mtandao huu wa Facebook, mwisho wa siku nina wajibika kwa chochote kinachotokea katika mtandao wetu”, mwisho wa kunukuu.

INAYOHUSIANA  Mitandao ya kijamii yazuiwa Ethiopia kupisha mitihani

Ameahidi katika kufuatilia matatizo ya sasa na ya zamani amesema atafanya mambo yafuatayo:-

  • kuchunguza mitandao yote ambayo inashirikiana na uga wa Facebook kabla ya kufanyiwa mabadiliko ya mwaka 2014 ya namna ya kuweza kupata taarifa ya watumiaji,
  • kufanyia uchunguzi kazi za programu za kimitandao zinazotiliwa shaka na
  • kupiga marufuku mwanzilishi wa programu yoyote ambayo inagoma ama haitoi ushirikiano katika uchunguzi pamoja na hatua nyingine ambazo wanaona zitafanya Facebook kuwa mahali salama.
INAYOHUSIANA  Wiki mbili za ziada kwa watumiaji wa WhatsApp kwenye Blackberry 10 OS

Kufuatia kashfa hiyo kumeanzishwa kampeni ya kuwataka watu kufuta kabisa akaunti zao za Facebook kwa hashtag ya #deletefacebook.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.