Mtandao wa Youtube umetangaza kuleta matangazo mafupi yasiyokwepeka, mtandao huu ambao ndio ni moja ya majukwaa yanayotumiwa zaidi na watu kutazama video mbalimbali. Matangazo hayo kwa mujibu wa Google yatakuwa mafupi na yenye kuburudisha.
Hatua hii ya Youtube haijapokelewa vizuri na watumiaji wa mtandao huu, na wengi wameonesha kusikitishwa kwa mtandao huu kuzidi kongeza matangazo. Hata hivyo Google katika tarifa yake wameendelea kusistiza kwamba matangazo haya yatakuwa ni mafupi na yenye kuburudisha.
Matangazo ndiyo uti wa mgongo wa biashara ya Youtube kwa kuwa watumiaji hawachangii kuangalia video zinazowekwa, unachofanya mtandao huu ni kujitahidi kuhakikisha kwamba wanakuwa na watumiaji wengi wa kudumu (kitu ambacho wamefanikiwa mpaka sasa) lakini pia wanajaribu kuwasehemu ambayo matangazo yanaletwa kwa wingi zaidi ili waweze kujiendesha kibiashara.
Matangazo ambayo mpaka sasa yapo katika mtandao huu yanaweza kukwepeka pindi mtumiaji anapoamua kueyaepuka, kitakachotokea baada ya mabadiliko haya ni kwamba hatutaweza kusitisha tangazo mpaka pale litakapokuwa limefikia mwisho hii itawalazimisha watumiaji kuangalia video za matangazo mpaka mwisho kitu ambacho kwa wateja sio kizuri ila kibiashara kinamaana kwamba watu watalipa gharama kubwa zaidi kuweka matangazo katika mbtandao huu.
Matangazo haya mapya yanayokwenda na jina la bumper ads ambayo hayakwepeki sio kwamba yatayabadili matangazo ambayo tumeyazoea bali yatakuwa ni kama nyongeza. YT wanasema kwamba wataendelea kuleta matangazo katika ubunifu kwa kadiri ya namna jinsi watumiaji wanavyotazama video na kwamba watumiaji wategemee mabadiliko kuendana na mwenendo wa watazamaji wa video.
Kama wewe ni mfanyabiashara hii ni fursa sasa ukiweza kulipia na matangazo yako yakawa yanachezwa katika video za Youtube maana yake utawafikia watumiaji wengi zaidi, kwa watumiaji wa kawaida hii inaweza ikawa ni pigo kwa maana wengi hawapendezwi na matangazo lakini huu sio mwisho wa maisha kwani wahenga walisema bure ghari.