Kampuni ya Google imethibitisha kwamba kipengele cha mandhari ya Dark Mode kwa watumiaji wa YouTube kimeanza kupatikana kwa simu zenye kutumia mfumo endeshi wa Android.
Kipengele cha Dark Mode kilitangazwa kupatikana tangu mwezi Machi mwaka huu lakini kilikuwa kinapatikana kwa watumiaji wa simu za mfumo wa iOS. Kwa watumiaji wa kompyuta Dark Mode ilianza kupatikana tangu Mei 2017.
Kwa kawaida muonekano wa YouTube kwa muda wote umekuwa wa rangi Nyeupe (white background) lakini ujio wa Dark Mode mtumiaji atakuwa na chaguo aidha aweke Nyeupe au Nyeusi.
Ikiwa kwenye YouTube ya kwenye simu yako hutaona kipengele cha Dark Theme, basi jaribu kupakua masasisho na bado hutaona kipengele hicho basi kuwa mvumilivu kwani utakuwa bado haujawezeshwa.
Utumiaji wa mfumo-Dark Mode unasaidia sana kwenye utunzaji wa chaji kwenye simu kutoisha mapema zaidi ukilinganisha unavyoperuzi Youtube ikiwa kwenye ule muonekano ambao unafahaika na wengi.