fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Teknolojia

Makanisa kuwekwa Wi-Fi nchini Ujerumani

Makanisa kuwekwa Wi-Fi nchini Ujerumani

Spread the love

Makanisa ya Kiprotestanti maeneo ya kati nchini Ujerumani yatakuwa yakiwapa waumini fursa ya kuingia katika mtandao, kwa kuwawekea huduma ya wi-fi bila malipo.

Huduma hiyo itapatikana katika maeneo ambayo, kwa kufuata ‘hostpots’ ambalo ni jina la vitovu vya huduma, yamepewa jina “Godspots”.

SOMA PIA  Baada ya Kutumia Mabilioni, Jeshi la Marekani Lasita Utumiaji wa Roboti katika Ubebaji wa Mizigo

Huduma hiyo ya Wi-fi itawekwa katika makanisa 220 katika majimbo ya Berlin na Brandenberg. 

Kwa mujibu wa kituo cha runinga cha RBB, mpango huo baadaye utatekelezwa katika makanisa 3,000. Makanisa ya kwanza kupata huduma hiyo yatakuwa kanisa kuu la “French Cathedral” eneo la “Gendarmenmarkt” na kanisa la “Kaiser Wilhelm Memorial Church”.

makanisa

Kanisa la French Cathedral, Berlin litakuwa miongoni mwa makanisa ya kwanza kunufaika

 

SOMA PIA  Apple kutengeneza modem zake za 5G kufikia mwaka 2023

Watu wataweza kutumia huduma hiyo kutoka ndani na nje ya kanisa. Wanaotumia huduma hiyo watakutana na ukurasa wa tovuti yenye maelezo kuhusu kanisa lenyewe, jamii ya eneo hilo na maelezo ya kidini. Lakini pia wataweza kutembelea mitandao mingine pamoja na kudownload chochote.

Una mtazamo gani juu ya kahuduma haka ka intaneti kutoka eneo la ibada? Pia haijajulikana kama tovuti ovyo kama vile za ngono zitaweza funguka kama kawaida kwenye huduma hiyo.

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia.

Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comment

Comments

  1. […] Soma Pia – Makanisa Kuwekwa WiFi nchini Ujerumani […]

TeknoKona Teknolojia Tanzania