fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

Teknolojia

Teknolojia kuua ajira nyingi kufikia mwaka 2030. Fahamu sekta zitakazokua. #Tafiti

Teknolojia kuua ajira nyingi kufikia mwaka 2030. Fahamu sekta zitakazokua. #Tafiti

Kwa muda mrefu kumekuwa na shutuma ya kwamba teknolojia itakuja kuua ajira za kwenye sekta nyingi katika mataifa mengi duniani. Utafiti uliofanywa kwenye baadhi ya mataifa unaonesha hilo jambo ni la kweli, ila sasa fahamu pia kwamba teknolojia pia itatengeneza ajira mpya nyingi kwenye sekta ya uchumi.

Utafiti uliofanywa na shirika la Boston Consulting Group (BCG) la nchini Marekani kwenye masoko ya ajira ya Marekani, Ujerumani na Australia umegundua ya kwamba hofu kubwa iliyowekwa dhidi ya teknolojia kupoteza ajira si sahihi. Wamekubali ya kwamba kuna mamilioni ya ajira zitapotea lakini kwa wakati huo huo ukuaji wa teknolojia utatengeneza ajira katika sekta zingine.

Kwa watafuta ajira kitu kikubwa kujiandaa ni kuhakikisha wanajifunza ujuzi sahihi kwa mahitaji ya ajira ya miaka hiyo ijayo. Na kama wewe ni mzazi basi pia ni kuhakikisha mtoto wako anaanza kujifunza ujuzi unaolingana na mahitaji ya miaka ya baadae.

Utafiti unaonesha katika miaka hii mikumi ijayo utumiaji wa teknolojia katika baadhi ya kazi nyingi ambazo zimekuwa zikifanywa na wanadamu utasababisha uharibifu wa nafasi za ajira nyingi zilizokuwa zinategemewa kabla. Lakini pia utumiaji huo huo wa teknolojia utazalisha ajira katika sekta zingine.

Teknolojia kuua ajira

Teknolojia kuua ajira mbalimbali miaka ijayo, ni vizuri kuhakikisha kama mfanyakazi unajiandaa kwa hili kwa kuongeza ujuzi katika maeneo yenye uhitaji zaidi

 

Sekta zitakazokuwa na nafasi za ajira zinazokua zaidi ni sekta zinazohusisha teknolojia za kompyuta, sayansi, uinjinia na hesabu. Pia maeneo ya huduma za afya, jamii na ualimu.

SOMA PIA  Tujue Kwa Ufupi Historia Ya 'KeyBoard' Na Wapi Tunapoenda Na Teknolojia Hii!

Sekta zitakazopoteza zaidi nafasi za ajira ni pamoja na sekta za utunzaji na uwekaji wa rekodi/taarifa, wauzaji madukani/rejareja, manunuzi na ugavi, na sekta zingine zinazoshabihana ambazo utumiaji wateknolojia kwa sasa tayari unapunguza uhitaji wa wafanyakazi wengi kufanya kazi nyingi zaidi.

SOMA PIA  Fahamu maana na kazi ya CC na BCC kwenye barua pepe

Je una mtazamo gani juu ya hili? Tuambie kwenye comment, usisahau kushare.

Chanzo: ZDNet na vyanzo mbalimbali

Comrade Mokiwa

Comrade Mokiwa

Muanzilishi wa Teknokona na Teknokona Group LTD - WWW.TEKNOKONAGROUP.COM

Muda wangu umegawanyika kati ya kazi kibunifu @teknokonagroup na uandishi wa habari za Teknolojia hapa Teknokona Blog.

| mhariri(at)teknokona.co.tz |

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania