Dunia ya leo vitu vingi tuu vimehamia kwenye ulimwengu wa kidijiti na kufanya mageuzi makubwa sana kuhusu sayansi na teknolojia ukilinganisha muongo mmoja, miwili iliyopita.
Ingawa maarifa mengi yamefichwa vitabuni lakini teknolojia inaweza kuweka vitu katika njia ya picha, maandishi ya kidijiti na hata picha jongefu. Vilevile, si jambo la ajabu mtu kuweza kujifunza kitu kupitia YouTube na akaweza kukifahamu/kukifanya vyema (mfano: Bw. Julius Yego-mwana michezo kutoka Kenya aliyeshinda medali ya dhahabu katika mashindano ya kurusha mkuki mwaka 2015) ambae alijifunza mchezo huo kupitia kuangalia picha mnato za mafunzo kwenye YouTube.
Je, ni kwanini wafuatiliaji na waangaliaji wana umuhimu mkubwa sana kwenye YouTube?
Kimsingi sababu kwanini watu hawa (wafuatiliaji na waangaliaji) ni muhimu sana ipo mojatu nayo ni kuwezesha kupata pesa (kulipwa) kupitia Youtube kama baadhi ya vigezo vilivyowekwa na wahusika (YouTube). Swali la pili utauliza “Kivipi?”. Kwa wale ambao hawafahamu kwamba Youtube inalipa watu iwapo akaunti zao ni za kibiashara, machapisho yao yana ubora (muonekano mng’avu) na bila kusahau wana wafuatiliaji/waangaliaji wa kiwango cha chini kilichowekwa na Youtube.
>Ili YouTube imlipe mtu kulingana na kile alichokiweka mbali na ambavyo nimeviorodhesha muda mfupi uliopita ni LAZIMA akaunti iwe na wafuatiliaji (subscribers) wasiopungua elfu moja (1000) na machapisho yako yawe yameangaliwa kwa saa zisizopungua elfu nne (4000) katika kipindi cha miezi 12.
>Pia, chaneli yako iwe imeunganishwa na akaunti ya matangazo” (AdSense) na uwe unaishi kwenye nchi/eneo ambapo programu ya “YouTube Partner” inapatikana.
Mpaka mwezi Agosti 2020 takwimu zinaonyesha YouTube inalipa wastani wa $3-$5 kwa kila waangaliaji 1000.
Mfano unaonyesha ni watu wangapi waliongalia kilichochapishwa kwenye Youtube katika kipindi cha siku 28.
KUMBUKA:
Wafuatiliaji ni watu ambao wanapata taarifa fupi mara tu unapokuwa umeweka kitu kwenye chaneli yako na waangaliaji wale wanaoangalia chapisho kwenye YouTube kwa sekunde zisizopungua kumi na moja (11) hadi thelathini (30).
Ni wazi kuwakupitia YouTube tunapata mengi mazuri basi ile sentensi “Usisahau ku-subscribe chaneli yangu” ni njia ya kukuomba umsaidie na yeye aweze kupata pesa mara baada ya kukuelimisha, kukuburudisha kupitia chapisho lake kwenye YouTube. Wahenga walisema “Kufa kufaana“.
Timu ya uandishi wa Kona ya Teknolojia ingefurahi kupata sapoti yako ili iendelee kukuletea habari na maujanja mbalimbali.
Wezesha bando kwa kutuma kiasi chochote kupitia Selcom, kwenye simu yako bofya *150*50*1# kwenye namba ya malipo weka 60751369 jina litakuja TEKNOKONA.
Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia.
Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|
No Comment! Be the first one.