Katika miaka kadhaa sasa makampuni mengi yamejaribu kutoka kompyuta mpakato ambazo zinaweza kutumika katika namna mbili tofauti; kutumia kama kompyuta au tabiti katika kifaa hicho hicho.
Smartron T-Book Flex ndio kompyuta/tabiti ambayo imetoka baada ya miaka miwili kupita tangu mtangulizi wake. Ni kifaa ambacho huwezi kuhisi karaha kutembea nacho kwani sio kizito kabisa na kumfanya mtu asiweze kufurahia pindi anapokuwa amekiweka kwenye mfuko.
Mchanganuo wa sifa za Smartron T-Book Flex.
Keyboard
Kwa mtu yeyote anayependa kutumia kompyuta mara kwa mara kwa shughuli zinazzohusiana na kuandika basi atapenda kuwa na kompyuta amabyo ina keyboard yenye vitufe vya kubonyeza imara na ndivyo ilivyo kwenye kompyuta/tabiti, Smartron T-Book Flex.
Tabiti
Umuhimu wa tabiti unaonekana pale ambapo unahitaji kifaa chako kwa matumizi ya kawaida sana na pengine unataka kutembea na kifaa hicho kwa urahisi zaidi.
Sifa |
Uwezo |
Prosesa | Zipo katika toleo mbili tofauti; Kizazi cha saba cha Intel Core m3 na Core i5. Kasi ya prosesa ni 2.4GHz na 5GHz mtawaliwa. |
Kioo | Kina ukubwa wa inchi 12.2, ubora wa picha: 2560×1600 pixels. Ina kalama maalum pia kioo kinaweza kuzunguka mpaka nyuzi 150. |
Diski uhifadhi/RAM | Ina GB 128 SSD pia unaweza kuweka memori kadi kadi. |
Betri | Betri yake ni Lithium-ion Polymer yenye 40Whr. |
Kamera | Ina kamera mbaili; kamera ya mbele ina MP 2 na ile ya nyuma ina MP 5. |
Programu endeshi | Inatumia Windows 10. |
Bei |
Core m3 ni $637| Tsh. 1,433,250 na Core i5 $ ni 786| Tsh. 1768,500 |
Usalama | Ina teknolojia ya fingerprint |
Wembamba | Ukubwa wa tabiti: 307.5 x 202.8 x 9.0 mm uzito wake ni gramu 950 bila keyboard na Kg 1.3 ikiwa na keyboard |
Sehemu ya kuchomeka spika za masikioni | Ina ukubwa wa 3.5mm |
Rangi | Machungwa, Kahawia, Nyeusi-Kahawia |
Teknolojia nyinginezo | Ina USB 3.0, USB Type C Thunderbolt 3 kwa ajili ya sehemu ya kuchaji, sehemu ya ziada kuchomeka keyboard ya nje, Wi-Fi Direct, and Bluetooth 4.0. |
Kompyuta/tabiti, Smartron T-Book ndio hiyo sasa wewe kama mdau wa teknolojia kifaa hiki kimekuvutia na pengine hata ukaamua kukinunua?
Vyanzo: Gadgets 360, mitandao mbalimbali
One Comment
Comments are closed.