fbpx

Roboti atakayeweza kushiriki tendo la kujamiiana! #Teknolojia

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +

ICT CONFERENCE 2019

Sambaza

Teknolojia ya roboti ambayo kila mara ina mengi ya kushangaza dunia mathalani roboti kutomika kwenye mapokezi hospitalini, roboti mwenye uwezo wa kupika ‘burger’, n.k. Sasa wataalamu wa kutengeneza roboti wanafikiria kuja na roboti mwingine atayekuacha mdomo wazi.

Roboti atakayeweza kushiriki tendo la kujamiana: Hili jambo limewagawanya watu wengi, tayari kuna midoli (wanaserere) inayotumiwa na watu kwa tendo la kujamiiana na sasa inaonekana watu wanataka kuyapa uwezo wa kiroboti zaidi na hivyo kuwa na akili na uwezo wa kujenga uhusiano kabisa.

INAYOHUSIANA  Apps za wanyama zawekewa katazo kulinda usalama wa wnyama pori

Kuna ule usemi unaosema “Ukistaajabu ya Mussa utaona ya firauni”, basi kama mdau wa teknolojia nathubutu kusema usemi huu kwenye makala hii umetimia. Usishangae kuona miaka kadhaa ijayo roboti atayekuwa na uwezo wa kufanya mapenzi 😯  😯 .

Nini chanzo cha uvumi huo?

Katika mkutano wa pili uliofanyika katika chuo kikuu cha Goldsmith mjini London baada ya serikali ya Malaysia ambayo ndio iliyokuwa taifa mwandamizi wa mkutano huo kuupiga marufuku. Hata hivyo, hakukuwepo na wawakilishi kutoka kwa sekta ya ngono wala roboti za ngono katika mkutano huo.

INAYOHUSIANA  Samsung yaweka rekodi kwa kupata faida ya mamilioni ya dola ndani ya siku moja

Kampuni ya Real Dolls inayotengeza wanaserere wa ngono ilidai kwamba itatengeza roboti wa ngono aliye na akili bandia mwaka ujao na iwapo uzinduzi huo utafanyika utakuwa ushahidi wa David Levy ambaye amekuwa akitabiri ujio wa roboti zinazofanana na binadamu zenye akili bandia.

Tuna roboti za urafiki na sasa roboti ambaye anaweza kuwa mpenzi ndio lengo jipya

Katika kipindi cha miaka 10 ijayo, inawezakana kutengeza roboti ambayo watu wataihitaji kama mpenzi, yenye upendo, kuaminika, heshima na hailalamiki. Wengi watapendelea uhusiano huo wa roboti na huenda wakataka kufunga nao ndoa.

Mpango huo wa mpenzi wa aina ya roboti huenda akazua maswali kadhaa ya kimaadili, hususani wakati ambapo sheria italazimika kutambua roboti kama binadamu.

Kuna maswali mengi ambayo majibu yake yakastaajabisha mfano ungefunga ndoa na roboti? Na je, roboti anaweza kuwa na haki ya kupinga ndoa hiyo? Tuandikie maoni yako hapo chini.

Vyanzo: BBC, mitandao mbalimbali

Facebook Comments

Sambaza

ICT CONFERENCE 2019

Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.