fbpx
simu, Tanzania, Vodacom

Kifurushi cha Wiki: Cheka Zogo kutoka Vodacom

kifurushi-cha-wiki-cheka-zogo-kutoka-vodacom
Sambaza

Kuanziavodacom sasa tegemea kupata taarifa za mara kwa mara kuhusu vifurushi na gharama za mawasiliano kutoka makampuni ya simu na huduma zingine za namna hiyo kupitia Teknokona.

Kwa leo tunakuletea vifurushi na gharama za mawasiliano kutoka Vodacom. Kwa ufupi makampuni mengi ya simu siku hizi yanavifurushi vya aina nyingi sana na wakati mwingine ata watumiaji/wateja tunapata shida kuvielewa au ata kuvijua. Tutajitaidi kuelezea vifurushi vingi zaidi kila pale tunapoweza kupata taarifa zaidi. Taarifa za hapa tumezitoa kwenye mtandao wao na vyanzo vingine.

Cheka Zogo ni kifurushi kinachowapa wateja wa Vodacom muda wa dakika za kupiga simu kwenda kwa wateja wengine wa Vodacom kwa gharama ndogo zaidi ukilinganisha na pale ambapo mteja atapiga bila kujiunga.

Cheka zogo inakupatia vifurushi vya muda wa maongezi tu na ni wakutumika kuwasiliana na wateja wa Vodacom tuu. Vifurushi lazima vitumike ndani ya masaa 24. Gharama inakuwa ndogo zaidi ukilinganisha na pale ambapo mteja atapiga bila kujiunga.

INAYOHUSIANA  VoLTE - Voice over LTE - Fahamu Kuhusu Teknolojia hii na utofauti wake na teknolojia ya sasa

Vifurushi vipo kama ifuatavyo;

i: Dakika 30 kwa Tsh 495/=

ii: Dakika 45 kwa Tsh 645/=

iii: Dakika 90 kwa Tsh 995/=

Kwa Ufupi (Unachopata)
-Vodacom kwenda Vodacom
-Dakika za maongezi pekee

Je ushawahi kutumia kifurushi hichi? Kumbuka kutufuata kupitia Twitter – Bofya na Facebook – Bofya

 

 

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Mhariri Mkuu

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. | mhariri@teknokona.com |

Reply your comment

Your email address will not be published. Required fields are marked*