Na Brian L. Anderson
Ulimwengu wa vitumi vya mkononi unakua kwa kasi kubwa na sii ajabu leo au kesho, wewe au mwenzako akanunua simu au tableti mpya na ukakutwa na swali la msingi sana – Niweke programu gani kwenye simu/ tableti yangu?
Swali hili ni la kwanza kati ya mambo mengi ya msingi ya kutatua ili kuhakikisha kitumi chako kipya kinafanya maisha yako yawe marahisi zaidi.
Kwa kutambua hilo, iwe simu au tableti yako ni ya Android, Apple ama Windows, tunakupa orodha ya programu ambazo kila mtu anatakiwa kuwa nazo ili kufurahia teknolojia ya mkononi kwa mambo tofauti.
Orodha hii imeandaliwa mahsusi kukusaidia kushusha kwa haraka na uhakika programu muhimu kwa kitumi kipya na itakuwa ikisasishwa (updated) mara kwa mara punde tuonapopata programu nyingine muhimu na pia kutoka kwa maoni ya wasomaji.
Kwa mambo ya kiofisi:
Microsoft Office – Programu hii maarufu maofisini sasa inaweza kupatikana bure kwenye vitumi vya kiganjani.
Wunderlist – Hii programu ni kwa ajili ya kupangilia mambo ya kufanya na kuyafuatilia huku ikihifadhi mipango hiyo mtandaoni (Cloud). Programu hii ni rahisi sana kutumia na inapatikana bure kwenye mfumo-endeshaji wowote wa vitumi vya mkononi.
Adobe Reader – Programu inayotumika na watu wengi duniani kwa kufungua nyaraka zilizohifadhiwa katika aina ya pdf.
Email (Barua Pepe) – Hii inaweza ikawa imewekwa tayari kwenye simu au tableti yako lakini kuna programu nyingine kama outlook.com, gmail na yahoo ambazo zitakuwezesha kufanya mambo mengi zaidi na barua pepe.
Kwa kuhifadhi data mtandaoni (Cloud):
Dropbox – Dropbox ni programu nzuri kwa ajili ya kufanya mafaili yako yajitume na kupatikana kwenye kila kitumi chako, iwe ni simu, kompyuta au tableti tofauti kwa haraka na urahisi.
Google Drive – Kama unataka kubaki katika ulimwengu wa Google, Google Drive inakupa uwezo mkubwa zaidi kwa kukupa uhuru wa kuchagua programu nyingine kama Google Docs za kutumia kuhariri mafaili yako ambazo utatumia mtandaoni bila kuweka kwenye kompyuta yako.
Utabiri wa Hali ya Hewa:
Bing Weather – Inawezekana hii programu kutoka kampuni ya Microsoft ni bora zaidi na ya kuaminika linapokuja suala la kutabiri hali ya hewa. Inakupa uwezo wa kuangalia utabiri wa wiki siku na hata wiki mzima.
AccuWeather – Kwa utabiri wa hewa wa kila siku.
Kutafuta Mafaili Ndani ya Simu:
ES File Explorer – Angalia mafaili yako kwenye kitumi chochote cha Android na pia fanya mambo kadhaa kusimamia simu yako kama kufuta programu na kushusha mafaili sehemu unapotaka.
Astro File Manager pamoja na Cloud – Ni programu nyingine kwa Android ambayo ina uwezo wa kutumia cloud moja kwa moja, kitu ambacho kinaiweka juu kidogo ya Es Explore.
Kuvinjari Wavuti:
Google Chrome – Kivinjari wavuti kutoka kwa Google.
Opera Web browser – Kivinjari kinachotumika na watu wengi zaidi Tanzania.
Tafsiri Lugha:
Google Translate – Tafsiri kwa ajili ya Android.
iTranslate – Tafsiri lugha kwenye vitumi vya Apple.
Bing Translate – Tafsiri kwenye vitumi vya Windows Phone.
Kuhariri picha/video:
Pho.to Lab – Hii inakuja na fremu zaidi ya 500 kwa ajili ya picha zako na ‘backgroud, ‘filter’, ‘collage’ na hata chaguzo za kubadilisha picha za uso wa binadamu kufanana na sura za wanyama.
Photo Express – Hariri picha kwenye Windows Phone.
Kwa ajili ya kucheza miziki na video:
Shazam – Vumbua nyimbo usizozijua kwa kusikilizisha simu yako kwenye spika, pamoja na kupata maneno ya miziki (lyrics) uipendayo.
VLC – Cheza kila aina ya midia na programu hii.
Kudumisha simu au tableti yako
CleanMaster – Programu namba moja kwa kuondoa mafaili yasiyohitajika yanayojaza kitumi chako bure.
Battery Manager – Ongeza muda wa kitumi chako kukaa na chaji na pia, ondoa mafaili yasiyohitajika.
Kwa ajili ya mitandao ya jamii
Hii tumekuachia wewe msomaji uchague – Facebook, Twitter, Instagram, Viber, Vine, Snapchat, LINE, Whatsapp, Kik, Tumblr, 6 Snap, Google+, Jamii Forums? Ni wewe tu.
Je, una maoni juu ya orodha hii?Una la kuongeza au lakupunguza? Tuandikie hapa chini kwenye ‘comments’ au katika kurasa yetu ya facebook hapa na twitter hapa.
No Comment! Be the first one.