fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
IPhone Maujanja

Kama iPhone Inazima Na Kuwaka Mara Kwa Mara, Njia Hizi Zinaweza Kukusaidia!

Kama iPhone Inazima Na Kuwaka Mara Kwa Mara, Njia Hizi Zinaweza Kukusaidia!

Spread the love

Watumiaji wa simu za iPhone amabao baadhi yao huwa wanakutana na matatizo juu ya simu zao huwa wana chaguo la kwenda kwa vituo vya kampuni ya Apple vya kutoa huduma ili vifaa vyao vikaangaliwe.

Hata hivyo inachukua muda na kama  kituo cha kutoa huduma kinapokuwa mbali basi kunakuwa na gharama zingine za usafiri na mbaya zaidi ni pale kifaa kinapokuwa kimemaliza warrant yake hivyo mtumiaji atalazimika kuingia mfukoni.

Tatizo ambalo linaonekana kujitokeza mara kwa mara kwa watumiaji wa iPhone ni kwamba simu zao hizo zinaonekana kujizima na kujiwasha (Restarting) mara kwa mara. Jambo hili limekuwa kubwa kiasi kwamba hata mtandao wa Tumblr  una ukurasa wa watu ku ‘tag’ “iPhone keeps restarting” ambao umejazika na watu wengi sana na wengi wao wakielezea kukasirishwa kwao kwa tatizo hilo.

SOMA PIA  Kipengele Hiki Kinaweza Okoa Maisha Ya Betri Ya iPhone! #iOS13

Kwa watumiaji wa iPhone waliopata tatizo hilo la simu kujizima zima, hizi ni baadhi ya njia wanazoweza fanya kabla hawajaamua kupekea simu zao kwa watoa huduma wa Apple.

Picha hii ya matoleo matatu ya simu za iPhone inaonesha ni kwa jinsi gani ukubwa wa simu umebadilika sana

Picha hii ya matoleo matatu ya simu za iPhone inaonesha ni kwa jinsi gani ukubwa wa simu umebadilika sana

  1. Kuboresha Program Endeshaji

Simu  ambayo inajizima zima inaweza ikawa ni kwa sababu inatumia progamu endeshaji (operating system) ya zamani hivyo inabidi kuiboresha (Update). Pia la muhimu ni kwamba hata Apps zote inabidi ziboreshwe kama kuna toleo jipya.

  1. Kufanya Hard Restart

Hii ni namna ya kuilazimisha simu kuji ‘restart’ , watumiaji wanaweza kujaribu njia hii kwa kubonyeza na kushikilia kitufe cha kuzima simu kwa sekunde 10 mpaka simu iji ‘resart’

  1. Zima Alafu Washa Data
SOMA PIA  Jinsi Ya Kutengeneza Neno Siri (Password) Imara!

Njia hii imefanya kazi kwa baadhi ya watumiaji. Kama ajabu jinsi inavyoonekana kwa kuzima Data ya internet ya iPhone kisha kuiwasha tena kwa iphone zile ambazo zilikua zinatatizo  la kujiwasha na kujizima liliweza kurekebishika

  1. Futa/Unistall App Mpya

Kujizima na kujiwasha inaweza ikawa imesababishwa na App mpya amabazo umezishusha (download) hivi karibuni. Kama tatizo hili limetokea baada ya wewe kushusha baadhi ya App basi zifute mara moja maana zinaweza kuwa ndizo zinazoleta shida.

  1. Reset iPhone (Futa Kila Kitu Katika iPhone)

Hii sio njia iliyoshauriwa kwa sababu sio suluhisho sahihi kwa tatizo. Lakini hata hivyo inaweza kufanyika bila kwenda kumuona mtaalam na pia inaweza tatua tatizo muda mwingine.Watumiaji ambao wapo tayari kutumia njia hii inawabadi kwanza kabla ya kuanza na njia hii waafanya back up ya taarifa zao muhimu kama vile namba za simu n.k. kwa sabababu katika kufanya njia hii taarifa za simu amabazo ziliongezwa na mtumiaji, zote zitafutika

  1. Badilisha Betri
SOMA PIA  Fahamu kuhusu Google Finance

Njia hii haiwezekani kwa watu wengi maana inahitaji ujuzi kidogo. Lakini kwa usalama zaidi teknokona inashauri  upeleke kwa wataalamu ukitaka tumia njia hii. Wapo waliobadilisha betri na tatizo la simu la kujizima na kujiwasha likatatuka.

Ukiona haya yote umefanya na tatizo bado limesalia, inabdi uwaone wataalamu wa Apple na hao kwa hapa dar wanafahamika kama iStore Dar. Kwa msaada zaidi na kutatua tatizo lako watakuwa wa kwanza kukusaidia. Usisite kutuandikia lako la moyoni kwenye boksi la comment hapo chini. Tungependa sikia toka kwako.

Hashiman (@hashdough) Nuh

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi.
Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comment

Comments

  1. Simu yangu ya huawei p6 inazima na kuwaka yenyewe

Leave a Reply

Your email address will not be published.

TeknoKona Teknolojia Tanzania