Je, una tatizo la kuamka asubuhi? Unataka kubadili jinsi unavyoanza siku? Tumia alamu inayowasha redio na utaona kwamba ni jambo la kuburudisha na pengine ulikuwa unalikosa!
Moja ya mbinu ya kuwa mjanja ni kukamata fursa zilizopo. Kuna kipindi tuliandika kuhusu kuangalia tv bure kwa kutumia simu yako na ofa za intaneti usiku. Siku hizi mitandao kadhaa inatoa ofa ya intaneti asubuhi. Unaweza kutumia fursa hii kujiamsha kwa kutumia alamu ya redio kama mbadala wa alamu ya kawaida. Kuna mbinu mbili hapa ambazo unaweza kutumia. Moja ni Kwa kutumia app ya Tunein na nyingine ni kwa app maalumu ya alamu.
TuneIN na App nyingine ya redio.
TuneIN ni programu maarufu ya redio, inayojulikana duniani kote na ni chaguo la mhariri (editor’s choice) kwenye soko la Google Play. Ili kutumia TuneIn kushituliwa asubuhi, chagua moja ya stesheni unazotaka-> bofya menu -> ingia ‘options’-> ‘set alarm’. Kisha, weka mpangilio unaokufaa wewe kwa muda wa redio kucheza, siku ambazo alamu huita, muda na ukubwa wa sauti ya alamu. Ukimaliza utakuwa umeweka mlio wa stesheni unayotaka.
App Maalumu kwa Alamu
Kwenye soko la Google Play kuna app kadhaa za kukuamsha kwa redio ila PocketBell ndiyo app niliyoona ina mvuto na uwezo mkubwa wa kuaminika. Utumiaji wake ni mrahisi. Ukiwa unajua kiingereza kidogo au kama una mtu anayejua, unaweza kutumia PocketBell. Hatua zake ni rahisi hata hivyo. App hii ina muonekano mzuri kupita zote pamoja na kuwa na chaguzo nyingi kama:
- Kuchagua kati ya muziki, milio ya simu na redio ya mtandao.
- Kutumia ishara za mguso kwa ajili ya kuzima na kusogeza mbele alamu.
- Kuzuia intaneti ya simu kutumika kwenye kuamsha na redio.
- Kuwasha wayalesi kwa ajili ya mlio wa redio ya intaneti.
Kuna faida pia ukitumia app kama PocketBell ukilinganisha na app kama TuneIn. Kwa sababu PocketBell ni app maalumu, ina chaguzo ya kutumia mlio wa kawaida wa simu punde inapotambua kwamba intaneti haipo na hivyo, haitaacha kuita. Kama intaneti haipo kwenye TuneIN, umekwisha! Haita-ita! Pia, unaweza kuzuia kifurushi chako cha intaneti kwenye simu kisitumiwe na badala yake itumike wayalesi ambayo pengine ina unafuu zaidi.
Soma Pia: Je Unataka Kuamka? Jua Kengere/Alamu bomba kwa Android!
Je wewe unatumia app gani kama alamu katika simu yako? Tungependa kusikia kutoka kwako.
No Comment! Be the first one.