fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
apps

Burudika Kuacha Kuvuta Sigara Na App Ya Kwit!

Burudika Kuacha Kuvuta Sigara Na App Ya Kwit!

Spread the love

Vilevi vingi kama mtu ukivianza inakua ni ngumu sana kuviacha kwani wengi wetu tunakuwa kama watumwa kwa vilevi hivyo.  Uvutaji wa sigara nao ni ulevi ambao upo kwa kiasi kikubwa sana hasa kwa maeneo yenye ubaridi.

Sigara licha ya kuwa na athari kadha wa kadha lakini ni moja kati ya biashara yenye faida sana. Watu wanakatazwa kila siku kuhusu uvutaji lakini kuacha ni shughuli. Kama ulikua unavuta sigara na ndio umefanikiwa kuacha bado kuna tatizo lililobakia nalo ni kuweza kujizuia na matamanio ya kuvuta tena.

Kujikinga na matamanio (arosto) ni vigumu sana lakini unaweza kujitahidi na kuachana nayo kabisa kwa kupata motisha wa kutosha. Uimarishaji chanya na burudani kidogo inaweza ikafanya zoezi kubwa la kuacha kuvuta sigara kuwa dogo kabisa. Hii inawezekana kwani kama unapata burudani (unaburudika) basi na siku nazo zinakimbia sana na unaweza shangaa ukamaliiza siku nyingi tuu bila hata kuvuta sigara

App ya Kwit inafanya kazi kama vile Gemu katika kifaa chako katika kuboresha mazingira ya kukusaidia kujidhibiti na hamu ya kuvuta na kuacha kuvuta kabisa. Utaweza kupata pointi na hatimaye kupiga hatua kadha wa kadha na hii itatokana na siku ambazo hujavuta sigara. unaanza kutumia App hii kama mtawaliwa na sigara na unamaliza kama mwachaji kabisa wa sigara

Muonekano Wa App Ya Kwit

Muonekano Wa App Ya Kwit

Ukiwa unaendelea utaona afya yako inabadilika na unaanza pata pointi nyingi, mfano katika daraja (level) la 5 kaboni monoksidi inatolewa mwilini *ndani ya gemu*

SOMA PIA  App ya Azam TV yaanza kupatikana rasmi

Kama bado ukiwa unataka faraja na vitu mbalimbali vya kutia moyo App hii ya Kwit ina kadi 200 zilizojaa maneno ya motisha tupu, ambayo yatakusaidia kuhakikisha unapata motisha wa kutosha.

Na kwa kupata faraja zaidi hata kwa wanaokuzunguka unaweza sambaza maendeleo yako kutoka Kwit kwenda katika mitandao ya kijamii. Hapa unaweza pata pongeza na hata kukosolewa na watu na kupewa moyo pia, lakini hii yote itategemea unaitumia App ya Kwit namna gani. Kama  maendeleo ni mazuri ni lazima utapata pongezi

Lakini pia kitu kikubwa unachopata kutoka App ya kwit ni taarifa muhimu zinazokuhusu wewe. Katika dashibodi ya Kwit utaona ni sigara ngapi hujavuta, kiasi gani cha pesa umeweza okoa na pia siku ngapi umeweza ongeza katika maisha yako…. burudani tosha

SOMA PIA  Siri: Programu ya Apple yaita ambyulensi kumsaidia mtoto

Video Fupi Ikielezea App Ya Kwit!

[iframe id=”https://www.youtube.com/embed/uudBc_kgr9Y”]

App ya kwit inapatikana katika AppStore kwa watumiaji wa iOs, watumiaji wa masoko mengine wakae mkao wa kula kwani itaingia mpaka katika masoko yao.

Kuvuta sigara licha ya kuwa kunapigwa marufuku bado kuna watumiaji wengi, njia nyingi za kuzuia hili tatizo zipo. Na hapa ndipo teknolojia nayo ilipochukua nafasi yake katika hili. Kuna App mbalimbali zinazopinga matumizi ya sigara Kwit ikiwa moja wapo.

Tuandikie sehemu ya comment hapo chini wewe unalichukuliaje swala zima la kuvuta sigara na unahisi kitu gani cha kiteknolojia kifanywe ili kupunguza ua kuondoa tatizo hili kabisa. Tembelea mtandao wako wa teknokona kila siku kwa habari kadha wa kadha zinazohusu teknolojia.

Siku Njema!

Hashiman (@hashdough) Nuh

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi.
Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

TeknoKona Teknolojia Tanzania