Twitter mbioni kuanza kutumia maeno zaidi ya 140. Hii limekua tatizo kwa watumiaji wengi wa mtandao wa twitter kwa mda mrefu. Kampuni la twitter limepata malalamiko na maoni mengi kutoka kwa watumiaji wa wadau mbalimbali wa mtandao huo wa kijamii.
Pengine ndio maombi hayo ya watumiaji wa twitter yanafanyiwa kazi. Kwa taarifa za haraka haraka inasemekana kuwa Tweets zitaongezwa na kuwa herufi 10,000 ambazo zitaku sawa kabisa na namba ya herufi zitakazotumika katika sehemu ya ‘direct Message’ -DM (meseji). Ongezeko hili la idadi ya maneno katika Tweets linasemekana kuanza kutumika mwanzoni mwa mwaka huu na hii ni kutoka katika vianzo mbalimbali vya habari za teknolojia
Japokuwa muongeaji rasmi wa mtandao wa kijamii wa Twitter Bw.Jim Prosser aligoma kuongea jambo lolote kuhusiana na fununu hizi.
JINSI ITAKAVYOFANYA KAZI
- Kama kawaida katika mtandao huo sehemu yake ya kuona Tweet za watu (timeline) utaweza kuona maneno 140 katika tweet kama kawaida lakini utaweza kuona maneno zaidi uki’click’ hiyo tweet
Mpango huu unafanyika ikiwa ni mpango madhubuti wa bwana Jack Dorsey ambaye ni mtendaji mkuu wa mtandao wa twitter, katika kuhakikisha twitter inapata watumiaji wengi na kuwa mtawala katika mitandao ya kijamii
Swala la maandishi yenye idadi ya manen0 140 limewatesa wengi kwani imekuwa ikiwalazimu waandike zaidi ya tweet moja ili kueleweka. Tena kwa wale wasioweza kujielezea ni shida tupu!
“Nimeipa changamoto timu yangu nzima iangalie kwa jicho la tatu katika kuangalia namna gani tunavyoweza kuufanya mtandao wa twitter kuwa bora zaidi katika ku’share’ na watu mambo mbali mbali yanayotokea – Alisema Bw. Jack Dorsey katika mkutano wa kampuni”
Inavyosemekana twitter imekua na ukuaji mdogo katika ongezeko la watumiaji wa mtandao huo. hivyo imewalazimu wafikirie ni namna gani ambayo wanaweza washawishi watu wengi wajiunge na mtandao huo wa twitter. Moja katika njia hizo inasemekana na kuongeza idadi ya maneno katika tweet itakua moja wapo
No Comment! Be the first one.