fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
apps Teknolojia

Jua Umefanya Nini Leo Mwaka Jana Na TimeHop – #App

Jua Umefanya Nini Leo Mwaka Jana Na TimeHop – #App

Spread the love

Kujua umefanya nini leo mwaka jana inaweza ikawa ni gumzo kwako sio?. lakini kwa kutumia App ya TimeHop hilo linawezekana. Ukiachana na mambo ya #TBT (throwback thursday) katika Instagram kuna mengi unaweza kugundua uliyofanya katika mitandao yako ya kijamii

Sio lazima uwe mpotezaji wa kumbukumbu kutumia App hii, kumbuka unaweza ukawa ulifanya mambo  fulani hivi na kumbukumbu yake ikakuletea kicheko katika siku yako. kwa mfano mimi nikiona Post zangu za facebook za mwaka juzi lazima nicheke, sijui wewe?

SOMA PIA  Kampuni za simu Uchina zafanya vizuri kimauzo

Maisha yanabadilika sana siku moja utakuwa unawanunulia watoto wako midoli, baada ya kumaliza utashangaa wanawanunilia watoto wao midoli, kumbukumbu ni muhimu sana. lakini kadri umri unavyozidi kwenda hata uwezo wetu wa kumbukumbu unapungua lakini kama una App spesheli inakuwa rahisi kwako kujua nini ulifanya wakati uliopita (mwaka Jana)

App Ya TimeHop Katika Simu Ya iPhone

App Ya TimeHop Katika Simu Ya iPhone

Kumbuka pia teknolojia imefanya mambo yote haya kuwa marahisi, ili kubaki na kumbukumbu unaweza chukua simu yako na kuanza kupiga picha au hata kuchukua video na kisha kutuma katika mitandao yako ya kijamii. baada ya kuzitupia katika mitandao hiyo ya kijamii ni mara ngapi unachukuaga mda wako na kuanza kuziangalia tena? …pengine ni mara moja moja au haufanyagi hivyo kabisa sio?

SOMA PIA  BBM Yaja Na Maboresho Kabambe

Kuna App inaitwa Timehop, kazi yake kubwa ni kukukumbusha kitu gani ulifanya mwaka jana kupitia mitandao yako ya kijamii, hapa App inaangalia picha, video na hata post za kawaida na kukumbusha.

Inachukua vitu facebook, instagram na mitandao mingine ya kijamii ambavyo ulivypost mwaka jana na kuvionyesha katika App hii kama kumbukumbu.

SOMA PIA  Bluetooth 5.0 - Kasi ya mara 2 zaidi, umbali wa mara 4 na ukubwa wa mafaili wa 800% zaidi

Timehop ina kuwezesha kuangalia picha hizo na pia hata kuzituma katika mitandao ya kujamii (kawa ulichokuwa unakifanya mwaka jana si cha ajabu)

Shusha  iOs, Android

Shusha App hiyo katika simu yako ya Android au hata ile ya iOS na uweze pata kumbukumbu zako kutoka mitandao ya kijamii mara tuu mwaka mmoja unavyofika. Jaribu App hii na tuandikie sehemu ya comment kuwa umeipokeaje? Tembelea mtandao wako pendwa wa TeknoKonaDotCom Kila siku. Tupo Nawe Katika Teknolojia

Hashiman (@hashdough) Nuh

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi.
Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

TeknoKona Teknolojia Tanzania